Makala hii inaelezea soko la Forex kwa undani kadiri inavyowezekana. Utajifunza misingi yote ya muhimu itakayokusaidia kuwa mfanyabiashara.
Natumaini makala hii itakusaidia kuwa mbobezi na sio kutengeneza tu kitita cha haraka. Bila msingi, maendeleo si rahisi.
Inawezekana kupata faida kwenye Forex? Swali hili linaulizwa na kila mtu mgeni katika soko la sarafu. Kama isingekuwa inawezekana, basi kusingekuwa na kesi za utengenezaji fedha katika viwango vya mabadiliko.
Makala inahusu mada zifuatazo:
Forex ni nini?
Forex (FOReign EXchange) ni soko la dunia la sarafu. Ni mtandao wa benki za kitaifa na za biashara, makampuni ya udalali, na mawakala wengine wa kiuchumi wanaojihusisha na ununuzi na uuzaji wa sarafu.
Soko la fedha za kigeni ni soko lenye mtaji mkubwa zaidi duniani. Mauzo yake ya kwa siku yanafikia Dola za Marekani trilioni 7. Ujazo huu umewezekana kutokana na asili na soko duniani na miamala ya mtandaoni.
Tofauti na masoko ya hisa, Forex haina kituo kimoja ndani ambacho biashara ya sarafu inafanyika. Kwa sehemu kwa sababu ya hii, inafanya kazi muda wote (isipokuwa mwisho wa wiki) na bila ya mapumziko, ambayo ni ya kawaida kwenye mabadilishano.
Miamala ya Forex imegawanyika katika:
- ua;
- biashara;
- bahati;
- udhibiti (unabebwa na benki kuu katika kudhibiti viwango vya ubadilishaji).
Ifahamu Historia Yako Ya Forex!
Pamoja na maendeleo ya biashara ya kimataifa mwishoni mwa Karne ya 16, watu walikabiliana na ukweli kuwa sarafu za nchi mbalimbali zina uzito thamani tofauti. Iliamuliwa kubadili kwenda kwenye fedha ya karatasi “inayofanana”, ambayo inaweza kubadilishwa kwa dhahabu katika benki. Kukaribia kwa kati ya karne ya 19, wazo la “kiwango cha mabadilishano kwa kuhusisha dhahabu” lilitokea. Hivyo kiwango cha dhahabu kilizaliwa.
Mnamo mwaka 1944, makubaliano maarufu ya Bretton Woods yaliwekwa sahihi kuanzisha Mfuko wa Fedha wa Kimataifa. Na kwa matokeo, Dola ya Marekani na paundi ya Uingereza zilikuwa sarafu za kimataifa.
Mnamo mwaka 1976, kiwango cha dhahabu kiliondolewa, na kiwango cha mabadilishano kilianza kufuata Sheria za soko za mgawanyo na mahitaji.
Tangu mwaka 1990, soko la Forex limekuwa likipatikana si tu kwa taasisi za kifedha bali pia kwa wawekezaji binafsi na wafanyabiashara. Baada ya miaka mitano, imewezekana kufanya biashara katika fedha za kigeni kupitia Mtandao. Hivyo, mwaka 1995 ukawa mwanzo wa kipindi cha kisasa cha Forex.
Muundo wa Soko la Forex
Mauzo makuu ya Forex yanatolewa na benki kuu na benki kuu za biashara.
Vipengele vikuu vya soko la FX ni ugatuaji na biashara ya-muda-wote. Forex ni soko la juu-ya-kaunta lisilo na kituo cha kati cha biashara. Mzunguko-wote-wa saa kwa biashara ya sarafu imewezekana shukrani kwa vipindi vinne vya biashara, kila moja ikienda kwa kingine ndani ya saa 24 za siku.
Ukubwa wa Soko na Mtaji
Benki kwa ajili ya Mikataba ya Kimataifa inasoma ujazonaa soko la sarafu la Dunia. Viongozi wa benki wanatoa mtaji wa Soko na ripoti ya ujazo wa biashara kila baada ya miaka mitatu.
Tangu mwaka 1989, mauzo ya kila siku yanakuwa kwa uwiano wa 25-30% katika kila kipindi cha ripoti. Mwenendo umebaki kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita.
2010 – $4 trilioni kwa siku;
2013 – $5.3 trilioni kwa siku;
2016 – $5.1 trilioni kwa siku;
2019 – $6.6 trilioni kwa siku;
2022 – $7.5 trillioni kwa siku.
Chanzo:Uchunguzi wa Benki kuu ya BIS Triennial.
Aina ya Soko la Forex
Aina tatu muhimu za masoko ya fedha za kigeni ni ya sasa, ya mbele na yajayo. Tofauti baina ya masoko ipo kwenye muda wa ufikiaji. Inaweza kufanywa papohapo au kwa tarehe maalum.
Fedha za Kigeni za Sasa
Katika soko la sasa, biashara inakamilishwa wakati wa muda wake wa mwisho. Kwa mfano, kama ukinunua euro saa 9:00 leo mchana, sarafu hii itaonekana mara moja kwenye akaunti yako. Wakati mwingine, hatua hii inaweza kucheleweshwa kwa siku moja au mbili.
Kuna aina tatu za Mikataba katika soko la Forex la sasa:
TOD. (leo). Rahisi zaidi. Malipo yanafanywa wakati wa siku.
TOM. (kesho). Malipo yanafanywa siku inayofuata ya muamala.
SPT. (spot or T+2). Malipo yanafanywa siku mbili za kazi baada ya kukamilika kwa biashara.
Kwa utatuzi ulioahirishwa, kiwango muhimu kinaongezwa katika kiwango cha biashara. Katika kesi ya TOM na SPT, kwa siku moja na mbili, kwa mtiririko.
Fedha za Kigeni Za mbele
Mkataba wa mbele unahusisha kuingia kuuza au kununua kwa biashara ya jozi ya sarafu kwa wakati ujao katika bei iliyoamuliwa mapema. Kwa mfano, umeingia katika mkataba ujao wa EUR saa 9:00 alasiri leo. Hii ina maanisha kwamba katika sehemu fulani ya wakati ujao, tunapaswa kununua, na muuzaji anapaswa kuuza katika kiwango maalum. Kwa hiyo, utapata faida katika tukio la kuongezeka kwa nukuu ya wakati ujao, na utapokea kiwango lilichokubalika cha “euros” zenye nafuu.
Muda wa nukuu za sarafu za dunia katika soko la Forex unaweza kufikia hadi mwaka mmoja. Kadiri muda wa mkataba unavyoendelea, ndivyo mtaji utakavyokuwa mdogo.
Soko la Forex la Baadaye
Utatuzi wa mkataba wa siku zijazo, kama mkataba wa mbele, unafanywa katika siku zijazo. Tofauti kuu ni kwamba tarehe ya utekelezaji wa mkataba wa siku zijazo imefafanuliwa kabisa. Pia, mkataba wa siku zijazo unaweza kuuzwa tena kwa mtu wa tatu, tofauti na mkataba wa mbele.
Vyama huchagua soko la siku zijazo ikiwa mnunuzi anataka kuhakikisha dhidi ya kupungua kwa bei ya mali na muuzaji dhidi ya ongezeko lake.
Kuna aina mbili za sarafu zijazo:
mikataba yenye sarafu ya malipo kwa dola za Marekani (kwa mfano, GBP/USD);
mikataba inayohusisha viwango vinavyoingiliana na sarafu nyingine (kwa mfano, USD/TRY).
Nini Inaendesha Soko la Forex
Katika Forex, mawimbi mbalimbali yanawezekana, yasiyoelezeka kwa mtazamo wa kwanza. Mara nyingi yanahusishwa na matukio ya kidunia ambayo yanaathuri uchumu wa Dunia.
Kiwango cha shughuli za benki kuu, taarifa kubwa za kiuchumi katika nchi zilizoendelea zaidi duniani, majanga ya asili, na mambo mengine yanaweza kuathiri nukuu za sarafu.
Benki Kuu
Kazi kubwa ya benki kuu ni kuhakikisha uimara wa sarafu ya nchi.
Mabadiliko katika viwango vya riba na muingiliano wa fedha za kigeni una athari kubwa katika nukuu za Forex.
Benki Kuu zinapandisha viwango vya riba kupambana na mfumuko wa bei na kuushusha ili kuchochea ukuaji wa uchumi.
Benki Kuu inaathiri moja kwa Mona kiwango cha mabadilishano cha sarafu ya nchi kwa kununua na kuuza sarafu kwenye Forex kuongeza au kupunguza kiwango cha mabadilishano kulenga thamani.
Wakati mwingine uvumi kuhusu muingiliano wa Benki Kuu unaweza kuathiri kiwango cha mabadilishano.
Ripoti ya Taarifa
Kama wafanyabiashara, tunavutiwa na matukio ambayo yana athari za maana katika nukuu kwa muda mfupi.
Mabadiliko ya muhimu ya thamani yanaendana na taarifa zinazoitwa zenye vipaombele. Hizi ni:
Viwango vya ajira/ukosefu wa ajira;
GDP (Pato la taifa) la nchi zilizoendelea;
Maamuzi ya riba za Benki;
Makutano wa kamati ya sera ya Fedha.
Unaweza kuchambua orodha, tarehe, na muda wa ripoti za habari katika kalenda ya uchumi ya LiteFinance . Unaweza kuweka muonekano wa taarifa zenye kipaombele pekee. Kama sheria, utolewqji wa habari nyingine hautambuliwi na soko.
Forex Ni Halali?
Biashara ya Forex ni halali? Wengi wanavutiwa na jibu la swali hili. Kumbuka, soko la sarafu ya fedha, pamoja na kazi za madalali wa Forex, zinasimamiwa na Sheria.
Sio lazima kwa madalali kuwa na leseni ya kuingia katika soko la ndani ya benki. Hata hivyo, madalali wenye leseni wanaaminika zaidi kwa sababu wanakaguliwa mara kwa mara, wanaweka mahesabu kwa uwazi na wana fedha ya kufidia.
Vyombo vikuu tatu zinatoa leseni kuthibitisha uaminifu wa madalali wa Forex:
Tume ya Biashara ya Bidhaa za Baadaye ya Marekani (CFTC) na Jumuiya ya Kitaifa ya Wakati ujao ya Marekani (NFA).
Mamlaka ya Maadili ya Kifedha ya Uingereza (FSA) na Tume ya Usalama na Uwekezaji ya Australia (ASIC).
Tume ya Usalama na Ubadilishanaji wa Fedha ya Cyprus (CySEC) na Mamlaka ya Huduma za Kifedha ya Malta (MFSA).
Nini Kinafanyiwa Biashara katika Forex?
Forex ni jukwaa la biashara kwa ajili ya mabadilishano ya sarafu moja kwa nyingine. Kulingana na umaarifi wa shughuli za mabadilishano (kwa mfano, mabadilishano ya EUR kwa USD), jozi za sarafu zinataarifiwaz ambazo ni vtyombo vikuu vya soko la fedha za kigeni.
Kununua na Kuuza Jozi za Sarafu
Vyombo vya pekee vya soko la fx jozi za sarafu ambazo zinaonesha thamani ya sarafu moja kulinganisha na nyingine. Kwa mfano, katika EUR/USD, thamani ya euro 1 itaoneshwa katika dola ya Marekani.
Jozi maarufu ambazo zinahusisha ujazo mkubwa wa biashara zinaitwa jozi za sarafu kuu, au kuu. Zilizobaki zinaitwa viwango vya mtambuka.
Sarafu Zinazofanyiwa Biashara Zaizi katika Masoko Ya Forex
Jozi kuu za sarafu zinahusisha EUR/USD, USD/JPY, GBP/USD, USD/CAD, NZD/USD, USD/CHF, na AUD/USD. Ndizi zenye mtaji zaidi, ndio maana mwenendo wake wa bei ni mlaini.
Viwango mtambuka ni jozi za sarafu tete zaidi. Kwa uwiano, zinatembea pips nyingi zaidi kwa siku, lakini nguzu ya faida yake inapunguzwa na mtaji mdogo USD/PLN, USD/SGD, USD/CZK, USD/NOK, na jozi nyingine ni za viwango mtambuka.
Nani Anafanya Forex?
Benki Kuu na benki za biashara, mifuko ya uwekezaji na pensheni, na makampuni makubwa yanayojihusisha na shughuli za kiuchumi ni washirika wa Soko la Forex, ambazo wanafanya mauzo ya biashara kuu. Taasisi hizi za fedha zinatumia Forex hasa kwa ubadilishanaji wa fedha za kigeni na kwa uchache zaidi ulanguzi.
Nani anayeifanya Forex:
Benki na taasisi za fedha za kimataifa;
Makampuni makubwa ya kibiashara;
Serikali na benki kuu;
Walanguzi na wafanyabiashara binafsi.
Mnyororo wa washiriki kwa wafanyabiashara binafsi unahusisha mtaji wa dalali wa Forex na mtoa mitaji.
Dalali wa Forex au muuzaji wa Forex ni taasisi ya fedha inayowapa wafanyabiashara uwezo wa kufanya biashara katika soko la fedha za kigeni. Dalali pia anampatia mfanyabiashara zana muhimu, pamoja na kituo cha biashara chenye nukuu za mtandaoni, akaunti ya biashara, ufikiaji wa uchambuzi, na uwezo wa kutumia kiinua mtaji.
Watoa mitaji, kama ilivyo Sheria, ni benki za kimataifa, ambazo ni wawakilishi wa Soko la fedha za kigeni. Wanatoa nukuu za jozi ya sarafu kwa dalali wa Forex.
Namna ya Kufanya Biashara kwa Wanaoanza?
Kuianza biashara ya Forex, unahitaji kujisajili na dalali, pakua kituo cha wateja na fungua akaunti ya mfano au akaunti ya biashara.
Faida kubwa na uwezekano wa hatari unategemea na ujazo wa miamala, ambao unaoneshwa kwa loti.
Namna ya kufanya biashara katika Forex? Wafanyabiashara wanapata ukuaji na kupunguza kwa nukuu. Kwa hiyo, kuna aina mbili za miamala:
Kununua au kufungua biashara ya juu;
Kuuza au kufungua biashara ya chini.
Kama wafanyabiashara watatabiri ukuaji wa baadae wa mali, ni muhimu kufungua biashara ya juu kupata faida. Kama ni kushuka kunategemewa, fungua biashara ya chini.
Tumia kizuia hasara katika kila biashara. Ulinzi huu wa agizi tutafunga biashara kama bei itaenda tofsuti na utabiri wa mfanyabiashara.
Dhana za Msingi
Kufanikiwa katika biashara ya fedha za kigeni, unahitaji kukuza muda wote mbinu zako za biashara. Hatua ya kwanza ni kujifunza maneno ya Msingi kama pip, loti, tofauti ya bei, kiinua mtaji, na mtaji.
Pip ni nini katika Forex?
Wafanyabiashara wageni mara nyingi huuliza pip ni nini katika biashara ya Forex na namna ya kutambua ukubwa wake. Pip katika Forex ni kiwango kidogo ambacho thamani ya chombo cha biashara kinaweza kubadilika. Kwa mfano, kwa GBP/USD pair yenye nukuu ya tarakimu-tano, pip moja = $0.00001.
Lot ni nini katika Forex?
Lot katika Forex ni kipimo cha kawaida kwa upimaji wa ujazo wa nafasi ya sarafu iliyofunguliwa na mfanyabiashara.
Kama mfanyabiashara ananunua EUR/USD kw ujazo wa loti ya 1, basi amenunua euro 100,000. Wafanyabiashara wengi wa Forex wanatumia kiinua mtaji na kufanya biashara kupitia madalali, hivyo wanahitaji fedha pungufu.
Tofauti ya bei ni nini katika Forex?
Tofauti ya bei ya Forex ni tofauti baina ya bei cha chini ya kuuza (“ask”) na bei ya juu ya kununua (“bid”).
Kama bid = 0.91437 na ask = 0.91440, tofauti ni pip tatu.
Tangu tunapotaka kununua katika bei ya ask (ya juu) na kuuza katika bei ya bid (ya chini), tofauti inapaswa kuongezwa katika mwenendo unaotarajiwa wa bei.
Kiinua Mtaji ni nini katika Forex?
Kiinua mtaji katika Forex ni uwiano wa fedha za mfanyabiashara na ujazo wa nafasi anaoufungua. Kiinua Mtaji kinaweza kuongeza uwekezaji kwa mara 10, 100, na hata 1000. Chaguzi hii inawaruhusu wafanyabiashara kufanya miamala katika soko la Forex kwa amana ndogo kuliko inayotakiwa kununua loti moja ya kawaida, ambayo ni, vipimo 100,000 vya sarafu.
Mtaji wa ukingo ni nini katika Forex?
Mtaji wa ukingo ni kiwango ambacho mfanyabiashara anahitajikw kuwa nacho kuendeleza nafasi zilizofunguliwa. Fedha hizi zinafungiwa katika akaunti ya mteja mpaka pale nafasi inapofungwa. Kiinua Mtaji kinavyokuwa juu zaidi, ndivyo inapaswa kuwa na fedha chache zaidi kufungua biashara. Hivyo, mtaji wa ukingo ndivyo utakavyokuwa mdogo
Aina Tatu za Uchambuzi
Katika Forex, wafanyabiashara hutumia mara nyingi aina tatu za uchambuzi:
Kiufundi. Lengo la uchambuzi ni bei ya chati.
Uchambuzi wa Msingi unajifunza viashiria vikubwa vya uchumi na habari.
Uchambuzi wa maoni ya Soko katika biashara za kuuza au kununua.
Uchambuzi wa Kiufundi
Katika uchambuzi wa kiufundi, mwendo wa thamani unaangaliwa bila ya kuhusisha sababu zinazosababisha.
Zana za uchambuzi wa kiufundi zipo chini:
Mfumo wa chati (kichwa na mabega, pembe tatu, bendera, n.k.) zinaunda mwendo wa bei.
Viashiria ni vyombo vinavyofanyiwa mahesabu kulingana na thamani ya bei. Vinamsaidia mchambuzi kuchuja ishara za uongo na kufanya utabiri sahihi zaidi. Wastani wa Mwendo na mizunguko ya stochastic ni kati ya viashiria maarufua.
Mifumo ya Candlestick inaoneshwa katika chati kama bei za mishumaa. Utabiri unahisi aina ya mshumaa na muunganiko wake, kwa mfano, baa ya pini au unyonyaji.
Uchambuzi wa Msingi
Uchambuzi wa Msingi wa Forex unachambua taarifa kubwa za kiuchumi ambazo zinaweza kubadili mahitaji na mgawanyo wa sarafu. Mara nyingi, utabiri huu ni wa muda-wa-kati na muda-mrefu.
Sababu za Msingi zinahusisha:
Habari na data zinazohusiana na hali ya uchumi katika nchi, ikihusisha ukosefu wa ajira na mauzo ya rejateja, fahisiri za bei ya wanunuaji, na maamuzi ya Hifadhi ya Shirikisho ya Marekani. Ni News and data relating to the economic situation in the country, including unemployment and retail sales, consumer price indices, and US Federal Reserve decisions. Ni rahisi zaidi kufuatilia taarifa hizi kupitia kalenda ya uchumi.
Matukio ya jiografia ya siasa kama uchaguzi, ushirikiano wa biashara baina ya nchi, na ushiriki katika miradi ya pamoja ya nchi.
Matukio yenye nguvu kidunia, ikihusisha majanga ya asili, mienendo ya kijeshi, na migomo..
Uchambuzi wa Maoni
Maoni ya soko ni uwiano wa kufungua biashara za kununua na kuuza katika chombo husika.
Kama ujazo wa manunuzi yaliyofunguliwa > ujazo wa mauzo yaliyofunguliwa, basi washiriki wengi wa soko wanatabiri ongezeko la bei.
Kama ujazo wa mauzo yaliyofunguliwa > ujazo wa manunuzi yaliyofunguliwa, basi washiriki wengi wa soko wanatarajia kupunguza kwa bei.
Nafasi zilizotangulia kufunguliwa haziathiri mwenendo wa baadaye wa bei. Kwa nyongeza, washiriki wakuu wa Forex ni benki ambao hufungua biashara si kwa sababu ya ulanguzi Bali kwa sababu wanahitaji sarafu fulani.
Aina ya Chati
Taarifa ya bei kwa vyombo vya Forex zinaoneshwa mara nyingi katika chati kama vifimbo vya mshumaa, baa, au mistari.
Fimbo za mishumaa zinaonesha zaidi hali ya chati. Zimeundwa katika pointing kuu nne:
bei mwanzo wa kipindi;
bei ya chini ya kipindi;
bei ya juu ya kipindi;
bei ya mwisho ya kipindi.
Baa zimeundwa kwa kutumia pointi nne pia. Aina hii ya chati unatumika na wafanyabiashara ambao wanahitaji kujua bei za juu na chini pekee kwa kipindi.
Chati ya mstari inahusika na bei ya mwisho ya kila kipindi au bei ya kufungua. Ni nzuri kwa kuchambua picha nzima lakini haipo vizuri kwa upande wa taarifa.
Wafanyabiashara wazoefu wanasoma miundo ya chati kwa uangalifu. Mifano mbalimbali inaweza kubashiri mgeuko wa bei na pointi sahihi za kuingia kwenye soko.
Chati za Vijiti vya Mishumaa
Chati za Vijiti vya Mishumaa zinaakisi myumbisho wa bei katika mfumo wa mishumaa ya Kijapani. Aina ya mishumaa unategemea na mabadiliko ya bei za juu na za chini za kipongi fulani:
kama bei ya kufungua ipo chini kuliko bei ya kufungua, basi mshumaa inaelekea chini (mara nyingi mweusi au mwekundu);
kama bei ya kufungua nipo juu kuliko bei ya kufungua, basi mshumaa unaelekea juu (mara nyingi mweupe au kijani).
Wakati wa kuchambua miundo ya fimbo za mshumaa, kuwa makini katika rangi za fimbo za mishumaa kutambua ishara zenye nguvu kwa kufungua biashara (kwa mfano, mmezo wa juu).
Chati za baa
Chati za baa zinaakisi vema bei za juu na za chini za chombo kwa kipindi kilichochaguliwa. Kufungua na kufungwa kwa vipindi kunaoneshwa kama mistari iliyolala kushoto na kulia kwenye baa, kwa mtiririko.
Chati ya baa inafaa kwa mambo ta chati na viwango vya bei.
Chati za mistari
Chati za mistari zinahusika na bei za muamala wa mwisho kwa kipindi kilichochaguliwa. Kwa mfano, katika chati ya mstari ya muda wa H1, kila alama inaakisi bei ya mwisho ya soko kwa saa iliyotangulia. Aina hii ya chati haitoi taarifa ya jinsi bei ilivyobadilika katika kila saa.
Namna ya Kutengeneza Fedha kwa Kufanya Forex
Wafanyabiashara wazoefu wanaotafuta taarifa ya namna ya kutengeneza fedha katika Forex mara nyingi hupata taarifa za uongo zinazohusikanna utabiri wa uhakika. Kwa matokeo hayo, wafanyabiashara wanapata uzoefu wa muhimu kwa mafanikio katika biashara yoyote lakini wanaangalia kwa urahisi njia za kutabiri bei.
Mifuko ya fedha wanatengeneza fedha kwa muendelezo kutoka kwenye biashara. Taarifa kuhusu faida zai inapatikana wazi. Kutokana na waanzilishi, mafanikio Yao yanategemea kwenye:
- mbinu za biashara ya faida ya sarafu;
- uwezo wa kuendana na Sheria za mbinu hii;
- usimamizi wa hatari unaolingana na kiwango cha mtaji.
Aina za maagizo ya Forex
Kuna aina za maagizo mbili katikaForex:
- soko;
- yanayosubiri.
Maagizo ya soko ya kununua na kuuza yanajumuishwa katika bei za ask na bid, kwa mtiririko. Hizi zinahusisha kununua soko na kuuza soko.
Maagizo yanayosuburi yanawekwa katika thamani fulani ya bei. Yatatekelezwa tu kama bei itafika katika thamani hizo. Maagizo yanayosuburi yamegawanyika katika aina mbili:
- Maagizo yenye ukomo yanaelekezwa kinyume na mwenendo wa bei (ukomo wa kununua, ukomo wa kuuza, kuchukua faida).
- Maagizo yenye ukomo yanayofuata mwenendo wa bei (kituo cha kununua, kituo cha kuuza, kizuia-hasara).
Wakatibwa Kununua au Kuuza Jozi ya Sarafu?
Kwa miaka michache ya kwanza, wafanyabiashara wa Forex walijaeibu kugundua wakati wa kununua au kuuza.
Hii ni kutokana na Dhana potofu kwamba mienendo ya soko inaweza kubashiriwa. Kwa muda, wakaanza kuangalia njia ambazo zitawaruhusu kutengeneza faida baada ya mfululizo wa miamala.
Kwa hiyo, kila manunuzi au mauzo yanafuata Sheria ya mbinu yako ya biashara.
Biashara ya Mfano Njia Yako kwenye Mafanikio
Wakati wa kufanya biashara katika akaunti ya mfano , wafanyabiashara wanafikia nukuu za soko bila ya kuhatarisha fedha halisi.
Faida ya akaunti ya mfano kwa biashara ya FX inadharauliwa sana. Kwa msaada wa akaunti ya mfano, watumiaji wanaweza kujaribu si tu mbinu za biashara lakini pia uwezo wao wa kuifuatilia katika masharti ambayo yapo karibu na uhalisia inavyowezekana.
Badili kutoka kwenye akaunti ya mfano kwenda akaunti halisi kama:
- matokeo ya jumla katika biashara 100 mfululizo ni karibu na 0 au chanya;
- umeendeleza mbinu ya biashara yenye sheria za wazi kwa kufungua na kufungwa biashara.
Saikolojia ya Biashara
Wafanyabiashara wanaoanza hawafahamu ushawishi wa hisia katika maamuzi yao. Hili ni tatizo kubwa linalohusiana na Saikolojia ya Biashara ya Forex.
Saikolojia ya wafanyabiashara inapaswa kuwekwa katika nukuu “Mimi si mwerevu zaidi”. Tunapaswa kukubali kuwa uwezo wa kubashiri una kikomo. Usiwe na makadirio ya juu kwa mahitaji yako kuhusu asilimia ya biashara za faida na kiwango cha kurudi.
Mtazamo huu kuelekea kufanya biashara unaboreshwa baada ya miaka Msingi ya mafanikio na makosa.
Cunaweza Kuwa Tajiri kwa Kufanya Biashara ya Forex?
Kuwa Tajiri kuna maana ya kupata fedha nyingi. Hivyo, umakini unahama mara moja kutoka kwenye kutaka kwenda kwenye kumiliki nyenzo.
Katika Forex, kama ilivyo kwenye tasnia nyingine, unaweza kuwa tajiri tu kwa kuwa mtaalamu.
Forex inawaruhusu wafanyabiashara kutumia kiinua mtaji kikubwa. Hivyo, kwa nadharia, unaweza kupata fedha nyingi siku moja wakati ukiuweka kwenye hatari mtaji wako wote. Hata hivyo, kumbuka kuwa aina hii ya biashara ya Forex ina faida tu kama ukiitumia kwa muendelezo.
Mbinu za Msingi za Biashara ya Forex
Mbinu ya biashara ya Forex, kama ilivyo sheria, unahusisha kufanya maamuzi yanayoendana na uchambuzi wa mwenendo wa bei ya mali.
Mbinu Bora ya biashara ya Forex inahisisha utambuaji wa tabia za miundo wa bei ambao unajirudia mara kwa mara. Mbinu kama hizi zinaonesha masharti ya kuingia na kutoka kwenye biashara ya Forex (kwa faida au hasara) ndani ya muundo wa bei.
Mbinu za biashara ya Forex zinaweza kugawamywa kulingana na njia ya uchambuzi na muda wa muamala.
Kulingana na njia ya uchambuzi:
- mbinu ya matendo ya bei;
- mbinu ya mifereji ya biashara;
- mbinu ya mwenendo wa biashara.
Kulingana na muda wa muamala:
- position;
- ndani ya siku;
- kukatakata;
- biashara ya kubembea.
Kuna mbinu za biashara ambazo haziangukiinkatika kipengele chochote, kama kubeba biashara, mtaji wenye kiziuizi, na ya moja kwa moja.
1. Mbinu ya Matendo ya Bei
Mbinu ya pekee ya mbinu ya matendo ya bei unategemea katika bei ya mshumaa mmoja au zaidi ya umbo fulani. Kila muundo wa tendo la bei inaakisi tabia ya wanunuzi na wauzaji kwa bei fulani kwenye wakati uliochaguliwa.
Matendo maarufu la bei ya baa ya pini na muundo mmezo yanaonesha nguvu ya kugeuka kwa bei kutokana na kuongezeka kwa ujazo wa biashara katika uelekeo kinzani wa mwenendo wa wakati huo.
2. Mbinu za Mifereji ya Biashara
Mbinu za mifereji ya biashara inahusika na mwenendo unaofanana na mawimbi. Kingo ya chini ya mfereji wa bei umejengwa na bwawaneo la chini la bei, wa juu ni kilele cha bei.
Mfereji unaweza kuwa wa kwenda juu au kushuka chini.
Biashara za Forex zinaweza kufunguliwa wakati bei imegisa tena kwenye kingo ya mfereji, ikitegemea mwendo zaidi kwenye uelekeo uleule.
3. Mbinu za Biashara za Mwenendo
Mbinu za biashara za mwenendo zinatumia viashiria vinavyoonesha Hali ya soko.
Kama ni mkusanyiko wa viashiria unapendekeza mwanzo wa uwezekano wa mwenendo wa juu, basi biashara ya kununua inafunguliwa. Kama viashiria vitaonesha mwanzo wa uwezekano wa mwenendo wa chini, biashara ya kuuza inafunguliwa.
Kama viashiria vitaonesha mlalp katika Forex, basi hakuna ishara za kuingia sokoni.
Tumia mbinu za mwenendo wakati vyombo vya biashara vina utete wa kiasi.
4. Mbinu ya Biashara ya Nafasi
Mbinu ya biashara ya Nafasi inahusisha kufungua biashara ya Forex kwa kipindi-kirefu. Kwa hiyo, vipindi vya muda mrefu kuanzia D1 na kuendelea vinatumika. Wafanyabiashara wa nafasi wanatumia uchambuzi wa kiufundi na wa Msingi kwa pamoja. Makadirio ya idadi ya biashara ni mpaka 10 kwa mwaka. Biashara zinafunguliwa kulingana na mwenendo wa muda-mrefu. Biashara katikati ya mipaka inapuuzwa.
5. Mbinu ya ndani ya siku
Kama sehemu ya kufanya biashara ndani ya siku, wafanyabiashara wanaweka biashara mpaka 5 kwa siku. Biashara zinafunguliwa katika muda fulani, wakati fulani wa biashara, wakati chombo kilichochaguliwa kina mtaji na utete wa kutosha.
Uwiano wa muda unatumika katika biashara ni kuanzia dakika 1 mpaka 60.
Kutokana na uchukuaji mdogo wa faida, matokeo yanaathiriwa na tofauti ya bei.
6. Mbinu ya kukatakata
Kutumia mbinu hii, wafanyabiashara wanahitaji kuwa na vifaa vya kutosha. Muda wa muamala ni kati ya sekunde kadhaa mpaka dakika kadhaa. Wakati wanategemea mwendo mdogo wa bei, ucheleweshaji mdogo (kutokana na muunganiko wa taratibu wa mtandao au ukosekanajinwa kitarakilishi chenye nguvu) unaweza kupunguza faida.
Mbinu ya Kukatakata inaweza kutumia wakati wowote wa biashara, wakati wote wa utete wa juu na chini. Kigezo kikuu ni udogo wa tofauti ya bei wa chombo.
7. Biashara ya kubembea
Vipengele vikuu vya biashara ya kubembea ni ubebaji wa nafasi zilizo wazo kwenda siku nyingine. Uwiano wa muda wa biashara ni kuanzia siku moja mpaka wiki kadhaa. Wafanyabiashara wanaobembea wanazewa kuchambua hata katika wakati mdogo kwa usahihi wa kuingia na uongezaji wa faida.
Kama sehemu ya mbinu hii, unaweza kukifanyia biashara chombo chochote kwani tofauti ya bei inawakilisha asilimia ndogo ya thamani ya faida.
8. Biashara ya Kubeba
Biashara ya Kubeba ni mbinu ya biashara isiyotegemea uelekeo wa bei. Inahusisha utangenezaji wa faida kutoka kwenye mahesabu yaalipo ya kulaza biashara (swap) wakati wa kubeba biashara iliyofunguliwa kwenda siku nyingine. Kulingana na tofauti ya riba za benki katika nchi mbalimbali, Makati ya kulaza biashara yanaweza kuwa chanya.
9. Biashara ya Mtaji uliozuiwa
Mbinu ya biashara ya Mtaji uliozuiwa sio mbinu ya biashara yenye sheria maalum kwa ufunguaji na ufunguaji wa biashara. Hii ni istilahi ya jumla kwa matumizi ya kiinua mtaji katika biashara ya Forex.
Mbinu nyingi katika Forex zinaashiria mipaka; tangu mabadiliko ya bei ya jozi za sarafuni madogo, faida zitakuwa ndogo kama itafanya biashara kwa fedha zako pekee.
10. Biashara ya moja kwa moja
Mbinu ya biashara ya moja kwa moja au biashara-ya-algo inahusisha matumizi ya roboti za biashara , programu maalum zinazofanya biashara zenyewe, bila ya uhusika wa wafanyabiashara. Aina hii ya biashara haihusishi AI kwani algorithm iliyojengwa-ndani unafanya maamuzi ya kufungua na kufunga biashara.
Mbinu za biashara za moja kwa moja zinaegemea zaidi katika biashara mlalo na zinatumika zaidi wakati wa utete wa chini.
Wakati Gani Unaweza Kulifanyia Biashara Soko la Fedha za Kigeni?
Wakati wa kufanya biashara ya Forex inapaswa kuchaguliwa kutokana na mpango wa jozi ipi ya sarafu unayotaka kuifanyia biashara. Muda mzuri wa kufanya biashara kwa sarafu kuu ni wakati wa saa za kazi wa taasisi za fedha Ulaya, Marekani, na Asia. Matukio ya biashara huongezeka wakati wa sarafu za Asia zinapiingiliana na kipindi cha utendaji wa Masoko ya Hisa ya Tokyo na Singapore.
Vipindi vya Biashara vya Forex Trading
Saa za biashara za Forex zinahusiana na vipindi vinne vya biashara:
- Pasifiki (22:00 - 06:00 UTC/GMT 0);
- Asia (24:00 - 08:00 UTC/GMT 0);
- Ulaya (08:00 - 16:00 UTC/GMT 0);
- Marekani (13:00 - 21:00 UTC/GMT 0).
Kipindi cha Tokyo
Masoko makubwa manne ya Hisa yanatoa utendaji katika kipindi cha Asia: HKE HONG KONG, SSE SHANGHAI, na TSE TOKYO.
JPY, SGD, na CNY zinafanyiwa biashara sana katika kipindi hiki, wakati jozi nyingine kubwa za sarafu zinakuwa na hali ndogo ya utete wakati wa saa hizi.
Kipindi cha London
Masoko makubwa manne ya Hisa yanatoa utendaji sana katika kipindi cha biashara cha Ulaya: LSE LONDON, SIX ZURICH, FWB FRANKFURT, na JSE JOHANNESBURG.
Wakati wa kipindi hiki cha biashara, jozi kubwa za sarafu katika Forex zinaonesha utete mkubwa kulinganisha na kipongi cha Asia. Utendaji wa EUR, GBP na CHF unaongezeka.
Kipindi cha New York
Kipindi cha biashara Marekani au New York kinaanza mara baada ya kipindi cha Ulaya kuisha. Kwa matokeo hayo, utete wa sarafu kuu unabaki kuwa juu.
Masoko makubwa matatu ya Hisa yanatoa huduma ya utendaji kwa kipindi cha biashara cha Marekani: CHX CHICAGO, NYSE NEW YORK, na TSX TORONTO.
Jozi, pamoja na USD na CAD, zinafanyiwa biashara sana kwenye kipindi cha Marekani.
Kipindi cha Sydney
Masoko makubwa ya Hisa mawili yanatoa huduma ya utendaji katika kipindi cha Pasifiki: NZX WELLINGTON and ASX SYDNEY. Jozi, pamoja na AUD na NZD, zinafanyiwa biashara sana.
Muda Mzuri wa Siku Kufanya Forex
Muda Mzuri wa biashara wa siku katika Forex kwa jozi kubwa za sarafu kwa upande wa mtaji na faida kubwa ni kwa kati wa vipindi vya Ulaya na Marekani.
Hata hivyo, wakati wa kuongezeka kwa hali tete kwa Kufanya Biashara ya Forex haufai kwa kila mtu. Kama wafanyabiashara wapo vizuri kwenye biashara Wakatibwa vipindi vya mlalo/au hali ya utete wa chini, basi ni vizuri kuchagua vipindi vya Asia na Pasifiki na chagua sarafu ambazo zinafanyiwa biashara sana kwenye vipindi hivi.
Mtaji wa sarafu fulani unategemea kipindi kilichopo. Kwa mfano, mtaji wa sarafu za Ulaya (EUR, GBP, CHF) unaongezeka wakati wa kipindi cha Ulaya, kwani vituo vya uchumi vya Ulaya vinakuwa wazi muda huu, na mtaji wa dola (USD, CaD) unaongezeka wakati wa kipindi cha Marekani. JPY na SGD zinakuwa na mtaji zaidi wakati wa kipindi cha Asia, wakati NZD na AUD zinakuwa na mtaji wakati wa kipindi cha Pasifiki.
BSiku Nzuri za Wiki za Kufanya Forex
Tofauti ya mwenendo wa soko kwa siku za wiki ni wa chini. Jumatano ina sifa ya kufungua kidogo kwa utete wa soko kulinganisha na Jumatatu na Jumanne. Ijumaa, bei huwa la mlalo. Hivyo, siku nzuri kwa biashara ya mwenendo ni Jumatatu, Jumanne na Alhamisi. Jumatano na Ijumaa zinafaa kwa biashara katika soko la ulalo na utete mdogo.
Kwa nini Kufanya Forex?
Kufungua akaunti ya Forex, inatosha ku jisajili na Dalali. Madalali wa Forex wanatoa nafasi ya kufanya biashara kwa ujazo mdogo wa kuanzia loti ya 0.01 na kutumia kiinua mtaji cha mpaka 1:1000. Kwa hiyo, unaweza kuzifanyia biashara baadhi ya vyombo kwa amana ya $50 au zaidi. Biashara ya Forex trading ipo wazi 24/5, hivyo wafanyabiashara wanaweza wasifuate utendaji wa vipindi kwa masoko fulani ya hisa.
Forex vs. Stocks
Kama tukilinganisha biashara ya Hisa vs. biashara ya Forex, soko la fedha za kigeni linashinda kwa tafsiri ya Mtaji, urahisi wa kufungua akaunti, na muda wa kufanya biashara. Soko la Hisa linafaa kwa tafsiri ya idadi ya vyombo maafueu, ukubwa wa tofauti ya bei , na uwazi wakati wa kufanya biashara.
Mtaji wa Forex unazidi mtaji wa Masoko yote ya hisa duniani. Kufungua akaunti ya Forex, unahitaji kujisajili na dalali. Kufikia biashara ya Hisa, unahitaji kutoa vifurushi vya taarifa.
Biashara ya Forex inafanyika muda wote. Hisa zina ukomo wa muda wa biashara.
Hisa za maelfunya makampuni zinafanyiwa biashara katika soko la Dunia la Hisa, wakati idadi ya sarafu katika Dunia ni mdogo.
Baadhi ya Hisa yumbishi zinaweza zisiwe na tofauti ya bei, ambapo ni tofauti na soko la Forex.
Kutokuweka kati kwa soko la Forex na uwekaji wa kati wa makampuni ya Hisa yanafanywa biashara kuwa wazi. Taarifa zote kuhusu ujazo wa biashara unapatikana kwa uwazi.
Forex vs. Zijazo
Tofauti kubwa baina ya Forex na soko la Hisa upo kwenye mkusanyiko wa vyombo vya biashara. Jozi za Sarafu zinafanyiwa biashara kwenye Forex, wakati Hisa na derivative mbalimbali kama zijazo, za hiari, na nyingine zinafanyiwa biashara kwenye soko la Hisa.
Tofauti na soko la Hisa, Biashara ya Forex inaendelea saa 24 kwa siku kwa kipindi kimoja kugeukia kipindi kingine. Wakati huohuo, Masoko yote yanafungwa Jumamosi na Jumapili.
Soko la Hisa linatoa kiinua mtaji (mpaka 1/10), lakini utete wa Hisa, zijazo, na vyombo vingine ni mkubwa kuliko wa jozi za sarafu. Hivyo, kiinua mgongo kikubwa kinahitajika hapa.
Pia, taarifa za ujazo wa biashara zinapatikana katika soko la kati la Hisa, tofauti na Forex.
Faida za Biashara ya Forex
Faida kuu sa biashara ya Forex:
- biashara inapatikana muda wowote wa siku;
- urahisi wa kufungua akaunti ya biashara ya Forex;
- mtaji mkubwa;
- kazi ya kiinua mtaji;
- fursa ya kujaribu mbinu yako katika akaunti ya mfano;
- biashara inawezekana hata kwa amana ndogo;
- orodha ya vyombo vya biashara pamoja na jozi za sarafu, vielelezo vya CFD, Hisa na bidhaa, fedha mtandao;
- vipindi vya utete-mkubwa na utete-mdogo vinabadilishana muda wote wa siku, ambavyo huruhusu wafanyabiashara watumie njia mbalimbali na mbinu;
- wigo mpaka wa vyombo bmbys madalali wa Forex pamoja na utabiri wa mali mbalimbali, kalenda ya habari za kiuchumi, ishara za biashara, na uwezo wa kuchambua miamala ya wafanyabiashara wengine.
Katika soko la Forex, uundaji bandia wa mahitaji na mgawanyo unawezekana, kama ujazo wa biashara ni mkubwa sana. Baadhi ya madalali wanatoa huduma kwa kunakili matendo ya wafanyabiashara wengine. Unaweza pia kuweka miamala yako kwa ajili ya kunakiliwa.
Kwa chati laini ya marejesho, hii inafanya uwezekano wa kuongeza amana kwa gharama ya fedha za wawekezaji
Hatari za Forex & Fursa
Ni muhimu kufanya tathmini ya kina ya fursa na hatari wakati wa kufanya biashara ya Forex:
Fursa | Hatari |
Kiinua mgongo | Ushawishi wa kubahatisha wakati wa kufanya maamuzi |
Tofauti ndogo ya bei na fursa za biashara ya muda-mfupi | Utelezaji na marudio ya nukuu |
Uwezo wa kuongeza amana mara kadhaa | Hatari ya kupoteza amana |
Ufikiaji huru wa elimu na nyenzo za uchambuzi | Usahihi wa utabiri wa uchambuzi si wa 100% |
Tuchunguze madhara ya hatari.
- Uwezo wa kufanya biashara kwa kwa msisimko kutumia mtaji wote uliozalishwa kwa mkupuo. Wafanyabiashara wa Forex wanaoanza hawawezi kutambua kiwango cha ushawishi cha silika na hisia katika hatua ya biashara kwa kuwa hawajakumbana navyo. Hatari ya kufanya maamuzi ya hisia katika sehemu ya kwanza, na ni ngumu kuizuia. Kiinua mtaji kinaweza kuwa cha hasara kwa wafanyabiashara kama, katika juhudi za kutengeneza fedha, hawakufuata Sheria za usimamizi wa hatari. Kwa upande mwingine, kiinua mtaji linafaa kupunguza kiwango cha amana.
- Hatari ya kuteleza na kurudia kwa nukuu ina maanisha kuwa agizo halijaingia katika bei iliyotarajiwa. Hii ni kutokana na kubadilishana kwa vipindi vya chini na juu vya mtaji katika chombo. Kuepuka hatari hii, tumia kalenda ya uchumi na usifanye biashara kwa kutarajia utolewaji wa taarifa muhimu za soko. Wakati wa vipindi vya mitaji mikubwa, wafanyabiashara wa Forex wanaweza kuweka biashara za kukatakata kwa kuwa ukubwa wa tofauti ya bei unafaa kwa aina fulani za akaunti.
- Hatari kubwa ya kupoteza amana inahusiana na kukiuka sheria za usimamizi wa hatari au kuhama kwa haraka kutoka kwenye akaunti ya mfano kwenda akaunti halisi. Haishauriwi kufanya biashara katika akaunti halisi mpaka matokeo yako ya mfano yakaribie sifuri au yawe chanya. La sivyo, akili yako inaweza isiwe tayari, na kuongezeka kwa maamuzi ya hisia. Kwa upande mwingine, kwa mbinu yenye uwezo, wafanyabiashara wanaweza kuongeza amana mara kadhaa.
- Inawezekana kujua nukuu za mbele kwa kutumia njia yoyote ya uchambuzi. Hatari za utabiri ulioshindwa zinaendana na asili ya mwenendo wa bei za Forex. Utabiri wa kichambuzi hauna dhamana ya kufanana na data halisi. Hata hivyo , unaweza kutoa muhtasari wa hali ya sasa ya uchumi mkuu inayohusiana na chombo cha biashara.
Wafanyabiashara wa Forex daima hufanya kazi chini ya hali zisizo wazi, hivyo unapaswa kupunguza hatari unazoweza kudhibiti.
P.S. Ulipenda makala yangu? Shiriki kwenye mitandao ya kijamii: itakuwa bora zaidi "asante" :)
Viungo muhimu:
- Ninapendekeza ujaribu kufanya biashara na wakala anayetegemewa hapa. Mfumo huu hukuruhusu kufanya biashara peke yako au kunakili wafanyabiashara waliofaulu kutoka kote ulimwenguni.
- Tumia msimbo wangu wa ofa BLOG kupata bonasi ya amana 50% kwenye jukwaa la LiteFinance. Ingiza tu msimbo huu katika sehemu inayofaa huku ukiweka akaunti yako ya biashara.
- Gumzo la telegramu kwa wafanyabiashara: https://t.me/litefinance. Tunashiriki mawimbi na uzoefu wa biashara
- Kituo cha Telegramu chenye uchanganuzi wa hali ya juu, hakiki za Forex, makala ya mafunzo na mambo mengine muhimu kwa wafanyabiashara https://t.me/litefinance
Biashara ya Forex FAQs
Biashara ya Forex unahusisha hatari. Matumizi ya maagizo ya kizuia-hasara na kufuata Sheria za kudhibiti hatari (si zaidi ya asilimia 1 ya amana kwa kila biashara na nyingine) itafanya biashara ya Forex kuwa salama iwezekanavyo.
Ndio, Forex ni Bora kwa wanaoanza kwa sababu ya sababu kadhaa. Kwanza, ni rahisi kujisajili na kufungua akaunti yako. Pili, unaweza kufanya biashara katika akaunti ya mfano na bila ya kuweka fedha halisi. Tatu, Ina mahitaji ya kuweka amana ndogo. Madalali wa Forex pia wanatoa ufikiaji wa nukuu za jozi maarufu za sarafu na fahirisi za CFDs, hisa na bidhaa.
Kwa kuingiza biashara za kununua au kuuza. Wafanyabiashara wa Forex wanajaribu kununua mali wakitegemea ongezeko la thamani yake kwa wakati ujao au kuiuza kama bei yake inaelekea kushuka. Kama utabiri utakuwa sawa, wafanyabiashara watapata faida, hivyo, tofauti chanya baina ya bei ya kununulia mali na bei yake ya kuuza (kwa kesi ya biashara ya juu)
Ndio, kadiri bei za mali zinazofanyiwa biashara katika Masoko ya fedha zinavyoendelea kupanda na kushuka. Kwa nyongeza, masharti ya madalali wa Forex yanaboreshwa, tofauti ya bei inapungua, idadi ya vyombo vya biashara inakuwa, na mawasiliano na watoa mitaji yanakuwa thabiti zaidi na zaidi.
Ndio, kama utaitazama biashara ya Forex kama mchezo wa bahati. Madalali wanatoa kiinua mtaji wa wafanyabiashara wa sarafu, inayotumiwa ambayo wafanyabiashara wanahatarisha kwa asilimia 100 ya amana yao katika biashara moja. Mazingira haya yanawezekana kama ukitumia Sheria rahisi za kudhibiti wa hatari.
Malengo yanategemea na washiriki wa soko. Kwa wafanyabiashara binafsi, hii ni faida imara inayotokana na matokeo ya miamala iliyokamilika. Lengo la benki ya biashara la benki kuu ya nchi ni kudhibiti viwango vya ubadilishanaji.
Hii inamaanisha kufungua kwa biashara kulingana na Sheria za usimamizi wa hatari na mbinu za biashara. Wafanyabiashara wanapasqa kuwa na mtazamo wa mtazamo kuwa maamuzi yao yanahusishwa uchambuzi, sio kazi ya kubahatisha.
Wafanyabiashara wageni wanafuzu haraka ufundi wa kufungua biashara katika Forex. Hata hivyo, kujiendeleza kwa mbinu zako binafsi za faida kwenye biashara kinaweza kuchukua miaka.
Hata kidogo, unaweza kufanya biashara katika Forex kwa kutumia akaunti ya mfano. Mahitaji ya amana ya chini katika akaunti halisi yanategemea na mali za chombo cha biashara (thamani ya pip1, mahitaji ya mtaji wa ukingo, kiinua mtaji) na ujazo wa biashara iliyopangwa.
Ndio, kwa mafunzo, unahitaji kujifunza chati ya bei na kupata elimu ya Msingi kuhusu kufungua biashara katika Masoko ya fedha. Kila kitu kingine kinakuja kutokana na mazoezi.
Ndio, wakati wa kufungua biashara ya Forex, kuna uwezekano wa matokeo ya faida na hasara kwani bei inaweza kubadili uelekeo muda wowote.

Maudhui ya chapisho hili yanaelezea maoni ya mwandishi na hayaelezei nafasi ya umuhimu kwa wakala LiteFinance. Nyenzo zilizochapishwa katika kurasa hii zimetolewa kwa nia ya kuto taarifa pekee na hazipaswi kuhusika kama ushauri wa uwekezaji kwa maleno ya Muongozo wa 2014/65/EU.
Kutokana na sheria ya hati miliki, chapisho hili linahusika kama elimu mali, inayohusisha katazo la kunakili na kusambaza bila ya idhini.


































