Kama unavyojua, kwa sasa kuna aina kuu 4 ya masoko ya kimataifa (mabadilishano ya hisa, bidhaa, sarafu na sarafumtandao). Si kwa kipindi kirefu kilichopita, biashara katika masoko ya fedha yalikuhitaji uwe na akaunti tofauti kwa kila mabadilishano. Tamaduni ya biashara katika hisa za makampuni ya kigeni haikuwezekana kutokana na sheria.
Hata hivyo, baada ya mawakala wa Uingereza kuja na Mkataba kwa Tofauti, kila mtu anaweza kufanya biashara popote pale kwa kuwa na akaunti moja ya biashara ya CFD kwa wakala mmoja wapo.
Hii ni kwa sababu CFDs sio mali peke yake, ila ni mpango wa tofauti ya bei. Kwa mkataba huu, unaweza kupata tofauti ya bei kutoka muda wa mkataba kusainiwa mpaka muda unafungwa, na haumiliki mali yenyewe.
Hii inafanya mikataba ya CFD kuwa rahisi zaidi, nafuu, na rahisi zaidi kuliko biashara ya jadi katika viwango vya baadaye au chaguzi.
Makala inahusu mada zifuatazo:
- CFDs ni nini (Mikataba kwa Tofauti)?
- CFD Inafanyaje Kazi kwa Mifano
- Namna ya kuanza Biashara ya CFD
- Mbinu za Biashara ya CFD kwa Wanaoanza
- Mbinu za Biashara ya CFD kwa Wataalamu
- Faida & Hatari za CFD
- Majukwaa ya Biashara ya CFD & Zana
- Sheria & Dondoo za CFD
- Biashara ya CFD vs. zana nyingine za fedha
- Hitimisho
- FAQ za Biashara ya CFD
CFDs ni nini (Mikataba kwa Tofauti)?
Hebu tufafanue CFD. Huu ni ufafanuzi wa CFD:
CFDs ni zana tata ambazo ni aina ya miamala kati ya pande mbili kuhusu thamani ya chombo cha msingi katika wakati ujao, ambapo pande zote zinaamua kuweka viwango sawa kati ya tofauti ya bei ya biashara ya kufungua na kufunga.
Kwa hiyo CFD ni nini? Ngoja nijaribu kuelezea maana ya CFD kwa undani. CFD ni ‘’mkataba kwa Tofauti’’, na ni mkataba au manunuzi kati ya muuzaji na mnunuzi lenye lengo la kutengeneza faida kutoka kwa tofauti ya baadaye kati ya bei za kufunga biashara na kufungua biashara.
Kama bei ya kufunga biashara ipo juu kuliko bei ya kufungua, muuzaji analipa tofauti kwa mnunuaji, na kama bei ya kufunga ipo chini ya bei ya kufungua, mnunuzi analipa tofauti kwa muuzaji.
Na kwa hakika, tangu mkataba wa CFD ni matokeo ya chombo cha fedha, kwa nyongeza ya tofauti yenyewe, pia inaratibu muda kipindi tofauti hii inaamuliwa.
Awali, kazi kuu ya mkataba kwa tofauti ilikuwa kuliifanya soko la hisa lipatikane. Na tangu hisa za CFDs ndizo maarufu zaidi, tutaangalia nafasi ya CFD katika biashara kama mfano.
Tuseme unataka kununua Mikataba ya hisa 100 ya Kampuni ya Boeing. Thamani ya hisa moja ni $160. Ili ununue hisa zenyewe, utahitaji kuwa na $16,000.
Lakini wakati wa kununua mikataba ya hisa za CFD, huhitaji kuwa na kiwango chote katika akaunti ya biashara ya CFD, utahitaji kuwa na mtaji. Wakala wa CFD LiteFinance ana mtaji wa 2% katika hisa.
Hivyo kununua loti 100 za hisa ya #BA (Kampuni ya Boeing), Utahitaji 2% ya 16,000, ambayo ni $320 pekee + kamisheni ndogo ya mabadilishano, ambayo bado hatutaichukua kwenye akaunti. Siku kadhaa zikapita na bei ya hisa ikapanda mpaka $170 kwa hisa. Bei imeongezeka, ikimaanisha muuzaji anapaswa kutulipa tofauti, ambayo itakuwa sawa kwa 170-160 = dola 10. Sawa tunaizidisha kwa idadi ya mikataba (100) na kupata dola 1,000.
Ni hivyo tu. Natumaini kuanzia sasa utaweza kuelewa maana ya Mkataba wa Tofauti.
Sasa tuangalie nini tunaweza kupata kwa kununua hisa zenyewe, na sio mkataba wa tofauti.
Fikiria tumenunua hisa 100 kwa $16,000, bei ikapanda mpaka 170 na thamani ya hisa zetu ikaongezeka mpaka 17,000. 17,000 - 16,000 = 1,000. Kwa hiyo, tumepata faida ile ile ya $1,000, lakini tunahitaji kuwa na $16,000 katika akaunti.
Kwa upande wa bidhaa za CFD, tunahitaji $320 pekee. Na kama hakuna tofauti — kwa nini kulipa zaidi? Hii ni ni faida ya msingi ya biashara ya CFD juu ya biashara ya mali yenyewe.
Kufupisha, ni wazi kuwa kwa mikataba kwa tofauti, tunaweza kufanya miamala ambayo haikuwa inapatikana hapo mwanzo kwetu kwa sehemu yoyote ya mabadillishano. Hatuhitaji kuwa na kingi katika akaunti ya biashara ya CFD kutengeneza faida kubwa.
Katika mfano wangu, tuna faida ya dola 1,000 kwa kuwekeza dola 320 pekee, na hii ni zaidi ya asilimia 300 ya faida ya uwekezaji iliyorudi, ambayo isingewezekana kwa kufanyia kazi mali yenyewe.
Biashara ya CFD ni nini
Ili kuelewa ni nini maana ya soko la CFD, kwa nini ni maarufu duniani na namna ya kuwa mfanyabiashara wa CFD, tuangalie historia yake.
Mikataba ya kwanza ilionekana London katikati ya miaka ya 90 ya karne iliyopita. Katika siku hizo, soko la dunia la Forex lilikuwa dogo sana na lilihusisha mabadilishano ya sarafu pekee: sarafu pekee ndizo zilikuwa zinafanyiwa biashara.
Nguvu kubwa ya biashara iliwekwa kwenye Mabadilishano ya Hisa, wakati mali halisi (hisa na dhamana) na dhamana za fedha zilikuwa zinashindanishwa kwa wateja.
Tangu soko la hisa lilikuwa ni moja ya masoko ya fedha na hakukuwa na chaguzi kwa wafanyabiashara wazoefu kwa wakati huo, serikali ilisimimia na kuweka masharti kadiri ilivyotaka. Sheria ya mabadilishano ilibadilika karibu kila mwaka, na makatazo makuu yalihusisha matumizi ya kiinua mtaji.
Hakika, sasa wote tumezoea kutumia biashara kwa kiinua mtaji na kubadilisha kadiri tunavyopenda, kuanzia 1:1 mpaka 1:1000. Hapo mwanzo hata kiinua mtaji cha 1:5 kilipatikana kwa mzunguko mdogo kwa vigogo wa fedha.
Kodi kubwa ya pili ilikuwa Ushuru wa Stempu. Kodi hii ililipwa kwa kamisheni kubwa katika manunuzi ya mali isiyohamishika, ardhi, pia hisa, dhamana na zana nyingine za uwekezaji.
Sababu hizi kubwa mbili zimekuwa nguvu kubwa ya uendeshaji kwa wafadhili wadogo katika kutafuta suluhisho kuepuka makatazo haya.
Pia kampuni ndogo ya dhamana ya fedha Smith New Court ilipata suluhisho. “Kwa nini ununue hisa, uzisajili, ulipe kamisheni kubwa na kodi kama hatupendezwi na kampuni yenyewe, ila katika mabadiliko katika bei ya kununua na kuuza hisa zake?”
Na kampuni na huduma za kifedha ziliamua kuwawezesha wateja wake kufanya biashara si kwenye hisa pekee, lakini kununua na kuuza mkataba wa tofauti katika bei ya sasa ya soko kwa hisa hii. Na tangu mtoaji wa mikataba hii ilikuwa kampuni ya huduma ya kifedha yenyewe, ilikuwa na haki ya kuziuza kwa kiinua mtaji chochote ambacho mteja alikihitaji.
Hapo mwanzo, wawindaji wa muda-mfupi wa mikataba walipendezwa na zana mpya, lakini baadaye wawekezaji wakubwa walizingatiwa kuwa umakini kufanya biashara na hisa za CFD. Iliwaruhusu kuepuka kulipa kodi kubwa, tangu hapo hakukuwa na umiliki halisi wa mali husika.
Mwishoni mwa miaka ya 90, mlipuko wa makampuni ya teknolojia ulianza na mikataba kwa tofauti ilibadilika kwa kiasi kikubwa. Gerard na Intercommodities zilikuwa kampuni za huduma ya kifedha zinazotoa huduma ya biashara ya hisa za CFD kupitia Mtandao katika jukwaa maalum la GNI Touch. Huu ulikuwa mfano wa kwanza wa kisasa wa soko ya Forex ulivyoonekana.
Baada ya muda, biashara ya mtandaoni ya hisa za CFD ilianza kutolewa na makampuni mengine ya kifedha na watoa huduma wa CFD duniani kote.
Kwa kweli, mawakala wa mkataba kwa tofauti wa wakati ule waliunda soko lao wenyewe ambalo liliweza kufikiwa kwa urahisi na wafanyabiashara binafsi wa CFD, na haikuhitaji kuwa na utaalamu ili kulifanyia kazi.
Masoko tete ya CFD yaliwezesha kila mmoja kutengeneza fedha kwa tofauti ya bei bila ya kumiliki mali halisi. Pia ilikuwa kiokoa muda kwa sababu haikuhitaji usubiri mpaka ombi lako la kununua lipitie hatua zote kutoka kwa wakala wa CFD na ubadilishaji kwenda kwenye nyumba ya kusafisha na kuhifadhi.
CFD ni chombo cha dhamana ya fedha, kinachomaanisha kwamba kinahusika muda wote na baadhi ya mali zilizopo.
Mali za kwanza za CFD zilihusika kwenye hisa, na sasa kuna biashara ya mikataba ya tofauti kwa kila kitu ambacho kinaweza kuuzwa.
Kwa sasa, mpango wa CFD kwa joto la nje ulisajiliwa Marekani. Watu wawili walisajili bashiri zao katika njia isiyo ya kawaida, na aliyeshindwa alipaswa kumlipa mshindi kwa utofauti katika joto la hewa kutoka wakati mkataba ulipokamilika.
Biashara ya CFD ina faida nyingi kuliko biashara za kawaida. Inahusisha matumizi yasiyo na kikomo ya kiinua mtaji, miamala ya papo kwa hapo, na mitaji midogo ya CFD. Na mwisho, unaweza kuzifanyia biashara CFD kwa nafasi za kuuza, wakati hisa-zisizo na mtaji haziwei kuuzwa, unaweza kununua tu. Hata hivyo, usisahau kuwa biashara yenye kiinua mtaji inahusisha hatari kubwa na unaweza kufanya akaunti zako za uwekezaji kupoteza fedha wakati wa kuzifanyia biashara CFD.
CFD Inafanyaje Kazi kwa Mifano
Sasa tuangalie namna ya kuzifanyia biashara CFD. Ni vizuri tukatumia mfano halisi.
Kwa mfano, tumeamua kununua Hisa za Tesla (#TSLA) CFD. Kwa maoni yangu, sasa ni wakati sahihi wa kununua mikataba ya hisa kwa kampuni hii. Ilikuwa na anguko hivi karibuni, na kutokana na moja ya mbinu kubwa, ambayo nitaijadili kwa undani, ni busara kununua sasa.
Kabla ya kununua au kuuza kitu chochote, unahitaji kupima faida na hasara. Faida inahusisha, kwa hakika, fadia inayotegemewa, na hasara ni hatari kubwa zinazowezekana na ukubwa wa kamisheni na tofauti ya bei.
Kila kitu kipo wazi kwa faida, sasa tujadili hatari kubwa ya kupoteza fedha kwa undani. Njia ya haraka ya kuhesabu vigezo hivi ni kikokotozi cha mfanyabiashara. Unaweza kukitumia hapa:
Hatua ya kwanza ni kuingiza vigezo vya akaunti yako ya biashara ya CFD: aina ya akaunti, sarafu ya akaunti na kiinua mtaji cha akaunti. Nimeingiza vigezo vya akaunti yangu ya biashara ya CFD;
Sasa twende kwenye mipangilio ya biashara yetu ya baadaye. Chagua aina ya zana ya biashara, katika kesi hii ni ‘’Mkataba kwa tofauti wa NASDAQ’’;
Kisha, chagua mali inayohusika. Kama tulivyoamua ni hisa ya Tesla, alama ni #TSLA;
Kisha, weka ujazo unaokadiriwa wa biashara, au CFD ngapi tunataka kununua. Hapa utahitaji kujua ni mikataba mingapi ipo kwenye loti moja. Kwa hisa za CFDs, mara nyingi ni CDF 1= loti 1. Nimeamua kununua loti 100;
Weka aina ya biashara. Katika kesi yetu, hii ni kununua au ‘’ndefu’’;
Sawa tunaweka bei ambayo tunataka kununua. Tangu tulivyonuia kununua katika bei ya soko, inawekwa moja kwa moja;
Na sasa tunaweka bei tunayotarajia kuiona, Ninatarajia uwezekano wa ukuaji kuwa $460 kwa hisa;
Baada ya kuweka vigezo, tunaminya ‘’hesabu’’, na chini itaonekana vigezo vyote vya biashara yetu ya baadaye;
Kwanza, tuangalie bei ya eneo moja. Kwa ujazo wetu, itatugharimu $1;
Kisha, unaweza kuona mtaji. Hiki ni kiwango cha fedha ambacho kitahitajika katka akaunti yetu ya CFD kununua mikataba 100. Kama nilivyosema hapo juu, hatuhitaji thamani yote ya hisa, lakini sehemu ya 3% ya kiwango chote, ambayo inapigiwa mahesabu kama ifuatavyo:
Inayofuata ni tofauti ya bei ambayo tutailipa wakati wa kufungua biashara kwa ujazo wetu. Kama unavyojua, tofauti ya bei ni tofauti kati ya bei za kununua na kuuza, na inaonekana kama hivi:
Kisha inakuja makato ya kulaza biashara, kamisheni ya usiku kucha;
Na mwisho, kikokotozi kinatupatia makadirio ya faida yetu kutoka kwenye biashara iliyowekewa vigezo.
Kuna aina nyingine ya ada — kamisheni.
Kama unavyojua, mawakala wengi katika soko la biashara la ECN wana aina 2 za akaunti za wawekezaji, Classic na ECN. Kwa hakika, pia kuna akaunti za bure za mfano, ambapo unaweza kufanya majaribio ya biashara ya CFD, lakini hii ni taarifa tofauti kabisa. kwa ufupi, tofauti kubwa kati ya akaunti hizi za wawekezaji wa rejareja ni aina na kiwango cha ada, kama tofauti ya bei, makato ya kulaza biashara, na kamisheni.
Katika akaunti za Classic, tofauti ya bei ni kubwa kuliko ile ya akaunti za uwekezaji za rejareja kwa kuhusisha vitu viwili — tofauti ya bei ya mabadilishano na tofauti ya bei ya wakala.
Soko ni eneo la wazi la biashara na kila mmoja anataka kutengeneza fedha, sehemu ya mabadilishao na watoa huduma wa CFD kwa pamoja. Akaunti za ECN zinatumia tofauti ya bei ya soko ‘’ghafi’’ bila nukuu ya wakala, ambayo inavutia zaidi kwa wafanyabiashara wa CFD wanaofanya kazi kwa vipindi vya muda mfupi.
Lakini kwa sababu hii haimnufaishi wakala, wanalipisha kamisheni kwa akaunti hizi za rejareja za wawekezaji, ambazo huwa na kiwango kilichowekwa muda wote. Kamisheni hii ni tofauti kwa zana za aina tofauti. Kwa mfano, kuzifanyia biashara CFD kwa hisa ni senti 25 kwa loti.
Na sasa mtego wa udukuzi:
Picha ya kioo hapo juu inaonesha namna nilivyouza aina 2 za mikataba ya tofauti, moja wa hisa za Google na mwingine wa General Electric.
Tambua jinsi tofauti ya bei ya kuuza hisa za makampuni ilivyo. Lakini kitu cha kuzingatia zaidi ni kamisheni ya senti 25 kwa kila upande. Ijapokuwa, kwa hisa za Google, kamisheni hii ni 0.017% ya bei ya hisa, ambayo ipo chini sana. Lakini kwa General Electric, kamisheni ni 4.09%.
Kwa hiyo tunaona kuwa kuna faida zaidi kufanya biashara na hisa zenye gharama zaidi chini ya masharti haya. Kwa usawa, inatakiwa kufahamika kuwa akaunti za rejareja za wawekezaji ziliundwa pekee kwa ajili ya biashara ya CFD.
Kabla ya kufungua biashara, tukumbuke namna faida inavyotengenezwa wakati wa kufanya kazi na mikataba ya tofauti.
Katika biashara ya CFD tunapata faida kutoka kwenye tofauti ya bei ya kufungulia na bei ya kufungia biashara.
Kwanza, tuangalie ni nini kinatokea unaponunua CFD.
Picha ya kioo hapo juu inaonesha biashara ya kununua CFD ya NASDAQ.
Tangu bei ya kununua na kuuza mali husika na bei ya kununua na kuuza mkataba wa tofauti unafanana, faida na hasaara zitahesabiwa katika njia ya kawaida. Kitu chochote juu ya bei ya kununua kitatengeneza faida, na kitu chochote chini yake kitaleta hasara. Unaweza kufunga CFD muda wowote.
Wakati unachagua kuuza CFD, inafanana, ila kwa sasa utapata faida wakati bei ya kuuza au kununua mali husika ipo chini ya bei ya kuuza au kununua wakati biashara imefunguliwa.
Kitu kingine cha muhimu ni muda wa biashara ya CFD, na hapa nitaifananisha na dhamana inayotokana na mali ya karibu zaidi — zinazokuja na za hiari.
Kama unavyojua, moja ya vigezo vya muhimu vinavyoathiri faida wakati wa kufanya kazi na dhamana zinazotokana na mali ni muda wa biashara.
Katika picha hapo juu, nimefananisha CFD na mikataba ya baadaye pamoja na chaguzi kwa kipindi cha mwaka-mmoja.
Kama unavyoona, unapaswa kuhusisha zijazo na chaguzi kwa pamoja kwa kila robo ili usipoteze thamani. Unaweza kununua zijazo kwa mwaka mzima,mlakini bei ya kununua itakuwa juu kuliko bei ya sasa ya soko.
Inafanana na chaguzi. Lakini mikataba kwa tofauti ni chombo kisicho na kikomo tangu mali husika haijakomaa. Unaweza kutunza biashara yako kwa muda mrefu kadiri unavyoweza.
Sasa tuiangalie biashara.
Kwa uwazi, nimefanya biashara kwa wakati mmoja akaunti za uwekezaji za rejareja za ECN na Classic ili kukusaidia kuelewa tofauti inayoonekana katika masharti ya biashara.
Masharti ya biashara yanaweza kuonekana katika kichupo cha ‘’taarifa kuhusu zana’’.
- Tofauti ya kwanza na ya muhimu ni tofauti ya bei kati ya bei ya kununua na kuuza. Akaunti za ECN zinatumia tofauti ghafi ya bei bila ya nukuu ya wakala, na hii inaonekana wazi katika kioo cha picha hapo juu:ntofauti ya bei katika akaunti ya ECN ni pointi 75, wakati kwenye Classic ni pointi 94.
- Tofauti ya pili ni kiwango cha kiinua mtaji kilichowekwa kwenye zana, ambayo tutaiongelea baadaye, kiinua mtaji ni 1:50, na katika akaunti ya Classic ni 1:33.
- Tofauti ya tatu ni asilimia ya mtaji, ambayo inaamua mtaji unaotakiwa kwa biashara ya CFD. Katika akaunti za ECN, ni asilimia 2% ya thamani nzima ya mali husika, na katika akaunti za Classic, mtaji ni asilimia 3%, ambayo inahitaji kiwango kikubwa katika akaunti ya biashara.
Sasa tufanye biashara.
Nitafungua biashara za CFD katika akaunti mbili tofauti.
- Kwanza tunachagua aina ya biashara: tuliyopanga kununua.
- Hatua inayofuata ni kuweka ujazo unaotakiwa katika loti. Loti 1 ni sawa na hisa moja ya hisa hizi. Tunanunua loti 100. Bonyeza ‘’nunua’’.
- Baada ya biashara kufunguka, linganisha vigezo kati ya akaunti. Kufanya hivi, bonyeza katika eneo la hali ya biashara. Hapa unaweza kuona kwanza tofauti — mtaji. Kama nilivyosema hapo juu, asilimia ya mtaji wa biashara katika akaunti ni tofauti, na tofauti hii ya asilimia 1% inatugharimu zaidi ya $400 katika mtaji. Katika akaunti ya ECN ni pungufu na kiwango ni usd 845.18, katika akaunti ya Classic kiwango cha mtaji ni USD 1271.19
- Kufungua dirisha la vigezo, unahitaji kubofya katika nukta tatu kulia kwa kitufe cha ‘’funga’’. Usikosee la utafunga nafasi kwa bahati mbaya.
- Tofauti nyingine ya muhimu kati ya akaunti ni kamisheni. Kama nilivyosema hao juu, ni senti 25 kwa hisa. Tumenunua hisa (mikataba) 100, ikimaanisha kuwa kamisheni itakuwa mara 100 zaidi, kuwa USD 25. Hakuna kamisheni katika akaunti ya Classic, na tumeokoa $25, lakini sio rahisi. Kama unakumbuka, akaunti ya Classic ina tofauti ya bei kubwa, ambayo mara nyingi hufidia kamisheni hii.
- Kwa matokeo, faida yetu ya sasa itaongeza tofauti katika nukuu na kamisheni. Fomula ya faida inaonekana hivi:
Kwa maneno mengine, nimenunua mikataba 100 ya hisa za Tesla. Bei ya kununua kwa pointi moja ni $1. Kama nilinunua ikiwa 400 na ikafunga ikiwa 410, faida yangu itakuwa: 100 * 1 * (410 - 400) = dola 1,000.
Baada ya muda, nilifuga biashara zangu za CFD, na faida kwenye akaunti zote zilikuwa zinalingana.
Kama nilivyosema, tofauti kubwa ya bei katika Classic ilifidiwa na kamisheni ya ECN, na tofauti pekee ilikuwa ni mtaji, ambao ulikuwa chini kuliko ECN.
Masoko ya CFD
Kama nilivyosema mara kadhaa, upeo wa mikataba kwa tofauti ni mpana sana.
Kwa sasa, kuna aina kuu 4 za mabadilishano (hisa, bidhaa, sarafu na sarafumtandao). Biashara ya CFD ipo kwa aina zote ya zana katika mabadilishano haya.
Njia maarufu zaidi ya kuzifanyia biashara CFD ipo kwenye hisa kwa makampuni maarufu zaidi, yanayoitwa ‘’vigae vya bluu’’.
Kwa nini? Tukumbuke namna mikataba kwa tofauti ilivyoundwa.
Kwanza kabisa, ni kwa ajili ya wawekezaji ambao hawawezi kununua hisa za makampuni ya kigeni kwa msingi wa sheria.
Kwa sehemu ya pili ni mikataba kwa ajili ya bidhaa kama mafuta, dhahabu, chai, gesi na nyingine nyingi.
Chaguzi ya tatu maarufu zaidi ni mikataba ya fahirisi za hisa.
Chini katika orodha hii ni CFD kwa ajili ya sarafu na sarafumtandao.
Nimeunganisha jedwali la mikataba kwa tofauti maarufu zaidi kwa aina ya mabadilishano.
Na pia, mtoa huduma wangu wa CFD LiteFinance ana zana zote katika orodha hii. Ni moja ya mawakala wa kwanza wa Forex kukupatia huduma ya biashara ya Forex ya CFD.
Namna ya kuanza Biashara ya CFD
Sasa tufahamu namna ya kuzifanyia biashara CFD. Hata hivyo, kabla ya kuingia kwenye soko husika, ni muhimu kufahamu kuwa biashara ya CFD inahusisha hatari na inaweza kukupelekea kupoteza fedha kwa haraka la uwe na uelewa mpana katika zana hii ya fedha.
Hatua ya kwanza ni kupanga mbinu. Inaweza kuwa ya dhahania au halisi katika mfumo wa maelekezo ya hatua-kwa-hatua. Kwa wale ambao wanapiga hatua yao ya kwanza katika masoko ya fedha, ninashauri kuweka mpango katika karatasi.
Upo tayari? Basi tuanze:
1. Kwanza kabisa, unahitaji kusajili akaunti na moja ya mawakala wa Forex.
Kwa nini Forex? Kwa sababu mawakala wa Forex wana wigo mpana wa mikataba kwa tofauti, ambao ni mpana kuliko unaotolewa na mawakala wa hisa na benki za uwekezaji.
Nimefanyia kazi maelekezo yangu kwa ajili yako katika akaunti yangu ya LiteFinance, ambayo ninayo kwa miaka mingi.
Kwa nini nimechagua kufanya biashara ya CFD na huyu mtoa huduma? Kwa sababu nimeridhika naye kwa miaka mingi.
Hata hivyo, sishauri kuanza biashara na fedha halisi. Ili kuanza hili soko na usipoteze akaunti yako ya uwekezaji wakati wa kufanya biashara ya CFD, itakuwa vizuri kuanza na fedha ya nadharia, ikimaanisha kuunda akaunti ya bure ya mfano.
2. Baada ya kuunda akaunti ya bure ya mfano, upo kwenye akaunti yako binafsi. Kushoto ni paneli ya wima, ambapo utachagua bidhaa ya kwanza ya menyu ‘’Biashara’’ na kubofya.
3. Kurasa ya biashara itafunguka, na sehemu ya chini ya kioo unaweza kuona baa ya kijivu ambayo sifuri (USD 0.00) inaonekana katika safu nne. Hii ni paneli ya kituo cha biashara, ambapo unaweza kutafuta historia ya fedha katika akaunti ya biashara. Sasa ni tupu kwa sababu akaunti yetu ya mfano haina kitu.
4. Kwanza unahitaji kuweka fedha kwenye akaunti yako. Kufanya hivi, bofya kitufe cha bluu ‘’Amana’’.
5. Kisha dirisha litaonekana katikati ya kurasa, lenye sehemu mbili. Kwanza, tunawezeshwa kufungua akaunti halisi. Sehemu ya pili kuna maeneo mawili; weka kiwango kinachohitajika sehemu ya juu. dola 10,000 za mfano zinatosha kwa kuanza.
6. Sasa bonyeza kitufe cha “Endelea’’.
7. Baada ya sekunde chache, salio halitakuwa 0.00, bali USD 10,000.
8. Ni muda wa kuanza majaribio. Kufanya hivi, bofya kichupo cha “Biashara” katika paneli kuu.
9. Menyu itaonekana juu, ambapo zana zote za biashara zimeainishwa kwa makundi. Kwa kuwa tunakwenda kufungua biashara ya CFD, tunapendezwa kwa kuanza na hisa, ikimaanisha tutachagua kichupo cha “Hisa” katika paneli.
10. Orodha itafunguka yenye hisa zote ambazo wakala anatoa mikataba kwa tofauti. Hapo mwanzo kwenye andiko, tulitaja hisa za CFD za Tesla. Kwa kuwa tunajua vizuri zaidi ya wengine, tufanye biashara ya CFD. Bonyeza katika jina la hisa au katika nembo.
11. Baada ya kubofya, dirisha la kufanyia biashara ya hisa litafunguka. Katikati ya kioo kutakuwa na chati ya bei ya hisa. Kama unafahamu misingi ya uchambuzi wa kiufundi, unaweza kuutumia.
12. Baada ya kuchambua tabia ya ya bei, nimeamua kwenda nayo juu. Hivyo tunaenda kwenye kichupo cha ‘’Nunua’’ sehemu ya juu kulia.
13. Katika mstari chini unahitaji kuweka ujazo unaopenda wa kununua. Ujazo wa chini ni loti 1 au hisa moja. Lakini kwa kuwa tuna USD 10,000, haitaleta maana kununua hisa moja. Nimeamua kununua hisa 100, au CFD za Tesla 100.
14. Baada ya kuangalia taarifa yote, tunahitaji kubofya “Nunua”, na ombi letu litakwenda kwa wakala na biashara ya CFD itafunguka.
15. Baada ya dakika chache, nimeona matokeo ya matendo yangu. Thamani ya eneo la chini la kituo imeanza kubadilika na bei imeenda juu sana, imeniletea faida ya $173. Kwa ufafanuzi, faida inaoneshwa kwa ukijani na hasara kwa wekundu.
16. Salio letu pia limebadilika katika eneo la kituo. Sasa sio 10,000, ila 10,148.
Sasa swali. Kwa nini faida yangu ni $173, wakati kipato halisi katika akaunti yetu ni $148? Jibu ni rahisi — kamisheni. Wakala amechukua kamisheni wakati biashara ilipofunguliwa, na inatolewa moja kwa moja kwenye faida. Kama unakumbuka, ni senti 25 kwa mkataba, au katika swala letu, dola 25, tangu tuna mikataba 100. 173 - 25 = 148.
17. Faida ya $174 inatosha kwa kuanzia, kwa hiyo tunaweza kufunga biashara yetu.
Kufanya hivi, bofya kwenye eneo ambapo salio linabadilika na kichupo kitafunguka juu kidogo kwenye biashara yetu au zetu. Tunatafuta iliyo sahihi na kutakuwa na kitufe cha “Funga” kulia kwake. Kibofye na biashara yetu itafungwa.
18. Faida katika akaunti ya mfano ni nzuri, isipokuwa hatutakuwa na matokeo halisi nje ya furaha ya mafanikio.
Kama umeamua kiukweli kujifunza namna ya kufanya biashara ya CFD kwa faida, unahitaji kuanza kutengeneza fedha halisi, na unahitaji akaunti halizi kwa ajili hii.
Kwanza, tubadilishe akaunti yetu binafsi kuwa ya biashara ya halisi ya CFD. Kufanya hivi, bonyeza kwenye ikoni ya wasifu kwenye kona juu kulia ya akaunti yako binafsi
19. Kichupo kidogo cha mpangilio kitafunguka, ambapo utahitaji kubofya kitufe cha “Wezesha Biashara ya Mubashara’’.
20. Baada ya kubofya kitufe hiki, hali ya akaunti itabadilika kuwa “Akaunti Halisi”. Sasa tunafanya safari ya umakini ya biashara.
21. Kwanza kabisa, tunahitaji kuweka fedha kwenye akaunti halisi. Kufanya hivyo, chagua kichupo cha “Fedha” katika paneli kuu.
22. Katika dirisha linalofunguka, katika menyu ya juu, chagua kipengele “Amana”.
23. Dirisha litafunguka na chaguzi za amana, kuanzia kwa kadi ya benki mpaka mifumo ya malipo ya kielektroniki. Unaweza kuchagua njia yoyote inayokufaa.
24. Baada ya kuchagua njia ya amana, unahitaji kuweka ombi la amana.
Eneo la kwanza litakuwa la kiwango cha amana.
Hali ya kila mmoja ni tofauti, lakini nitakupa dondoo moja. Nimefanya kazi katika masoko mbalimbali ya fedha kwa zaidi ya miaka 10 na nimekuja na suluhisho kuwa kiwango cha amana kinategemea tu na malengo unayojiwekea.
Malengo yote yanaweza kugawanywa katika aina 3: kujaribu, kucheza na kupata. Na “kucheza” sio utani. Baada ya kuhamia kwenye akaunti halisi, utani unaisha. Kwa sababu fedha yetu ipo hatarini na hatutaki kuipoteza.
Kujaribu. Chaguzi hii inawafaa wale wanaojaribu kuanza biashara yao katika masoko ya fedha.
Kama upo kwenye kitengo hiki, ili kuzifanyia biashara CFD, kuelewa namna zinavyofanya kazi na jaribu kujipatia mtaji wako wa kwanza. Kiwango mara mbili ya bei iliyochaguliwa kwenye hisa kinatosha.
Kwa nini bei ni mara mbili zaidi? Ili biashara moja au baadhi ambazo hazijafanikiwa zisiathiri amana yako sana. Katika suala la hisa za Tesla, ambapo hisa moja ina thamani ya $400, $1000 inatosha.
Kucheza. Chaguzi hii inafaa kwa wale wanaopendezwa na masoko ya fedha lakini hawana hamu ya kuingia katika ugumu wa nguvu ya biashara, kujifunza na kupiga mahesabu. Wanataka tu kununua hisa fulani kwa kiwango fulani cha fedha na kupata 100, 200, 300, au asilimia zaidi ya faida.
Unadhani huu ni uhalisia? Sivyo, lakini biashara hizo ni bahati kwa asilimia 99%, ndio maana kitengo hiki kinaitwa “kucheza”. Hata hivyo, ninajua mifano mingi ya uchezaji wa mafanikio.
Kwa mfano, turudi nyuma wiki 2 na tuuze CFD ya kampuni hii ya Tesla, ambayo ilikuwa ni $2,200 kwa hisa. Mikataba michache juu ya 100 ingeweza kuuzwa ndani ya siku moja na ingeleta $180,000.
Hii ni hadithi ya kweli, kulikuwa na wachezaji wachache wenye bahati tangu matarajio haya kuanguka mpaka sifuri. Kwa hiyo kama upo kwenye mtindo huu wa biashara, weka amana ya 1,000, 2,000, 3,000 au kiwango chochote unachotaka, bashiri fedha yote katika baadhi ya matukio na usubiri.
Kama ikitokea, utakuwa tajiri ndani ya siku moja, lakini kama haitafanya kazi, angalau umejaribu.
Kupata. Jina la kitengo hiki linajiongelea lenyewe. Hii ni njia ndefu na ya heshima ambayo muendelezo mwingi na malengo huweza kufuata. Mwisho wa njia hii hakika kutakuwa na malipo.
Mtu mmoja anaweza kuifanyia kazi mbinu yake ya faida na kuanza kujipatia kipato kwa muendelezo kwa msaada wa maarifa yaliyopatikana katika njia hiyo.
Mtu mmoja atatumia maarifa haya na uzoefu kufanya kazi katika eneo linaloendana na masoko ya fedha.
Mtu mmoja atapata uzoefu wenye thamani na kuamua kwenda kwenye njia ya kuanzisha kampuni ya uwakala.
Na mtu mmoja anaweza kuchagua njia niliyoichagua. Kwa nyongeza ya safari ya mafanikio ya biashara katika soko pekee, nimejikuta katika uchambuzi wa elimu na fedha.
Kama unataka kufuata njia ya kuwa mfanyabiashara halisi na kujifunza namna ya kutengeneza fedha, unahitaji mtaji mkubwa wa kuanzia na baadhi ya ujuzi wa mahesabu.
Mtaji wangu wa kwanza ulikuwa $4,000. Nimeandika tayari makala nyingi ambazo nimeongelea kwa ukubwa kuhusu gharama za biashara. Kwa hiyo kama unahitaji taarifa zaidi, tafuta makala zangu nyingine
Tuendelee. Leo nimechagua 4,000 kama mtaji wetu wa kuanzia kwa sababu biashara ya hisa inagharimu $400.
25. Baada ya amana, bonyeza kitufe cha “Biashara” na uone kiwango kinachohitajika kinachoonekana kwenye akaunti yako. Kitaonekana katika eneo la ‘’Fedha Zote’’.
26. Nina 4,852 badala ya 4,000 kwa sababu tayari nina salio la dola 852 kutoka kwenye utendaji wangu wa awali.
27. Tuanze biashara yetu ya umakini.
Tubonyeze katika kichupo cha “Hisa” na punguza mwendo kidogo. Kwa sababu tuna fedha halisi, maamuzi ya haraka si ya kwetu. Kwanza kabisa, tunahitaji kuchora kinachoitwa mpango wa biashara.
Unaweza kupata maandiko mengi kuhusu mipango ya biashara kwenye mtandao na kwenye blogu hii. Lakini kwa sababu nimeitaja, nitachora mpango mfupi wa biashara kwa ajili yako pia.
Mpango wa biashara ni muunganiko wa sheria ambazo unapaswa kuzifuata ili kufikia matokeo chanya. Na kwa msingi inaonekana kama hivi:
Mpango wangu wa biashara, ambao ninautumia sasa, una alama 37, na ninazijua zote kwa moyo. Hatua ya kutathmini mali muhimu inaweza kunichukua sekunde kadhaa mpaka wiki.
Kwa mtu anayeona mpango wa biashara kwa mara ya kwanza itamchukua kama saa moja kufanyia kazi alama moja. Lakini bila ya mpango wa biashara biashara zako za CFD hazitakuwa na mpangilio, na hatutaweza kuongelea kipato kilichotulia. Sitaingia kwa undani sana kwa kila alama ya mpango wa biashara, kwani nitatenga makala nyingine nje na hii. Tuelekee kwenye maeneo ya muhimu.
Ili kufanya uamuzi mzuri kufungua nafasi za juu au za chini, tunahitaji kuchagua muda wa kazi wakati zana inayofanyiwa biashara, kuchagua zana ya biashara, kawaida baada ya uchambuzi wa kiufundi au wa kimsingi, na usambazaji wa mtaji kwa ajili ya biashara.
28. Baada ya kuunganisha matamanio yako na mpango wa biashara, unaweza kuanza biashara. Bonyeza zana iliyochaguliwa. Kwa suala letu, zana yetu pendwa tena ni Tesla.
29. Kama tutabaki kwenye uchambuzi wa kiufundi, tunapaswa kuwa makini na bei ya chati.
Kuna aina nyingi za mbinu ya biashara, lakini moja inafanya kazi kwa wepesi — nafasi ya soko. Sitaingia kwa undani, kwa sababu nimeielezea mbinu hii katika moja ya makala zangu.
Wazo la jumla ni kuwa biashara imeanza na nafasi ya soko imetengenezwa, ambayo inatuelekeza kwenye mpando wa muda mfupi katika bei ya hisa kwa saa mbili au tatu zijazo. Muda unaisha na unahitaji kuchukua hatua.
30. Tangu soko limepanda bei, inamaanisha tutanunua. Tunaweka aina ya biashara kuwa “Nunua”.
31. Kisha tunaweka ujazo wa biashara. Nimeshafanya mahesabu ya mikataba 100 itanigharimu kama $900 katika mtaji wa CFD. Hii inakubalika kwa mtaji wangu wa kama 5,000, kwa hiyo nitanunua mikataba 100.
32. Baada ya kuweka vipimo, ninabonyeza “nunua”.
33. Na sasa nukuu ya pembeni kwa wale wasio wazuri sana na uchambuzi wa fedha na mbinu za biashara. Kuna eneo ya “Uchambuzi” kwa ajili yako; kitufe kinapatikana katika paneli yako kuu ya akaunti yako binafsi.
34. Katika diirisha litakalofunguka, bonyeza “Taarifa za Uchambuzi” na utafute zana inayotakiwa katika taarifa.I
35. Kuna mapitio ya Tesla hapo. Unapobonyeza, utaona mapitia ya kina ya uchambuzi ya moja ya wachambuzi wa kampuni na maoni yao katika zana hii. Unaweza kutumia hoja za muandishi na kufanya anayopendekeza. Lakini kwa baadaye nitasema kuwa ni vema utegemee maoni yako mwenyewe.
36. Wakati wa kuangaia kichupo cha “Uchambuzi”, mabadiliko yametokea kwenye bei ya chati. bei imeanza kupanda, kama tulivyotajaria.
37. Na sasa ni muda wa kuangalia paneli ya biashara kutathmini hali ya amana yetu. Wakati wa dakika 10-15 wa kusoma uchambuzi, bei ilipanda na kwa sasa biashara yetu imetupatia faida ya $560.
38. Natumaini hii ni inatosha kwa biashara ya dakika 10. Mbinu yetu imefanya kazi na tunapaswa kufanya haraka kufunga biashara yetu na kuchukua faida. Umekwisha fahamu tayari namna ya kufanya hivi, bonyeza kitufe cha “Funga”.
39. Baada ya biashara kufunga, ninashauri uifurahie faida yako ipasavyo. Kwa maneno mengine, unahitaji kuitoa faida na kuihisi kwenye mikono yako.
40. Hili ni zoezi la muhimu kwa wanaoanza na wafanyabiashara wazoefu, ambalo ni zuri kwa kujenga kujiamini. Kutoa faida kutoka kwenye akaunti ya biashara ya CFD nenda kwenye eneo la “Fedha”.
41. Ni kwa sasa tu, badala ya kichupo cha “Amana”, bonyeza kichupo cha “Utoaji”.
42. Tena, chagua njia ya utoaji.
Akaunti yako ya biashara ya CFD itaonekana katika uwanda na salio na kiwango kilichopo kwa utoaji. Nina 5,479. Kama unakumbuka niliweka 4,000, pamoja na dola 900 zilizokuwa kwenye akaunti. Jumla, nimeamua kutoa ziada yote juu ya 5,000. Dola 479 zinatosha kwenda kujinunulia zawadi kwa bidii na mbinu nzuri iliyofikiwa.
Mifano ya Biashara ya CFD
Baada ya kuchambua namna biashara ya CFD inavyofanya kazi na kwa mifano ya nafasi za CFD iliyooneshwa, tuhitimishe na kuangalia tena misingi ya muhimu wakati wa kufanya biashara ya tofauti.
Kitu cha kwanza kukumbuka ni namba CFD inafanya kazi, namna faida na hasara zinavyopatikana.
Baada ya kufanya maamuzi za kuanza biashara, tunapaswa kurudi kwenye mpango wetu wa biashara.
Baada ya kuamua zana ya biashara na vigezo, tunaamua kununua au kuuza. Matokeo ya biashara yatategemea moja kwa moja kama tumechagua uelekeo sahihi
Kuamua matokeo yanayotarajiwa ni rahisi. Hapo juu nimekupatia tayari mahesabu kamili ya fomula. Unahitaji kuzidisha tofauti ya bei ya kufunga na kufungua kwa bei ya alama moja katika ujazo wa chaguo lako.
Katika picha hapo juu, nimeamua kuachana na hisa na kukuonesha hili kupitia mfano wa mkataba wa mafuta ya Brent. Ni moja ya bidhaa maarufu katika mabadilishano.
Kwa mfano, tumeamua kununua mikataba ya mafuta. Mafuta yanauzwa kwa loti, na loti ya chini ni 0.1. Hata hivyo, tangu mikataba yenyewe kuwiana kwa unafuu, unaweza kununua kwa loti kamili au zaidi.
Kwa mfano wetu, nimenunua loti1. Bei ya kununua ilikuwa $40.00, na bei niliiuza kwa bei ya $45. Bei ya kuuza ipo juu kuliko bei ya kununua, hivyo nilitengeneza faida.
Kwa njia hiyo, ni alama ngapi bei imevuka? 500. Kwa nini?
Kwa sababu alama ni mabadiliko madogo ya bei kutoka kwenye soko la hisa. Kabla haijakuwa 45.00, bei ilipanda kutoka 40.00 mpaka 40.01, 40.02 na kuendelea, kubadilika kwa alama moja au zaidi.
Kwa hiyo faida ni sawa na: bei la alama (dola 1) kuzidisha kwa (bei ya kuuza (alama) toa (bei ya kununua (alama)), ambayo ni 1 * (4500 - 4000) = 500. Ni hivyo.
Kama hauna bahati na bei haijaenda juu, lakini muanguko wa soko ukatokea, nafasi yako ya kununua itatengeneza hasara. Itahesabiwa kwa kutumia fomula 1 * (3500 - 4000) = -500. Hasara katika suala hili itakuwa dola 500.
Tumepita kwenye hasara na faida, sasa tuangalie namna mtaji unavyofanya kazi.
Moyo wa biashara ya CFD ni mtaji wa biashara wa CFD, wakati mteja anapata kutokana na kiinua mtaji kinachotolewa na wakala. Tutaongelea kuhusu hili kwa undani hapa chini. Hata hivyo, ni muhimu kutambua kuwa biashara ya mtaji na kiinua mtaji ni upanga wenye makali kotekote, ikimaanisha kuwa inaweza kuzidisha faida yako, lakini, kwa upande mwingine, ikafanya akaunti zako za uwekezaji wa rejareja kupoteza hasara kwa haraka.
Ukopeshaji wa mtaji huweza kufanya kazi kwa viwango vikubwa vyenye mahitaji madogo ya amana katika akaunti.
Kwa hiyo, mfanyabiashara anaweza kufanya kazi na hisa au bidhaa na kutengeneza fedha kupitia hizo bila ya kuwa na kiwango kamili cha kununua mali husika.
Tuangalie namna inavyofanya kazi kwa kutumia mifano ya hisa za moja ya makampuni maarufu duniani — Google, or Alphabet Inc.
Thamani ya hisa moja kwa sasa inakadiriwa kuwa $1,445. Ili kuinunua, tunahitaji kiwango chote. Kwa kweli, hata zaidi pamoja na kamisheni na tofauti ya bei.
Lakini kama utaamua kununua si hisa yenyewe, bali CFD ya Google ambayo inalingana kwa ukubwa na hisa moja, hutahitaji kuwa na kiwango chote cha $1,445 katika akaunti yako, shukrani ka asilimia ya mtaji.
Mtaji kwa hisa hii ni 2% ya thamani nzima, au $28.98. Kwa maneo mengine, unaweza kupata hisa ileile, kwa unafuu zaidi. Faida yake itahesabiwa kama kawaida: alama ngapi zimetembea katika uelekeo wako ndio utakachopata.
Mbinu za Biashara ya CFD kwa Wanaoanza
Hii ni moja ya sehemu muhimu ambayo inajadili mbinu za biashara au mkakati wa tabia za soko.
Mkakati ulioelezewa vizuri utakusaidia kutengeneza fedha katika mienendo ya soko.
Kuna mikakati mingi ya biashara maalum kwa kufanya mazoezi ya biashara za mikataba kwa tofauti, lakini ninapendekeza uizingatie ya msingi na inayopatikana.
Biashara ya Juu & Chini ya CFD
Tuanze na mapitio ya mikakati ya kawaida ya CFD za Forex inayoitwa “nunua chini, uza juu”. Itaonekana kama hivi kwenye chati:
Picha hapo juu inaonesha chati mbili za mienendo ya soko kwa mali mbili tofauti.
Chati ya juu ni hisa za Facebook, na chati ya chini ni minada maarufu ya mtandaoni ya eBay.
Kama unavyoona, hisa za Facebook zilikuwa kwenye soko linaloshuka kwa muda mrefu na kwa sehemu ilifikia uwiano wakati bei ilianza kwenda chini. Wakati huu unaitwa usawa wa ugavi na mahitaji. Mara nyingibei ya hisa hubadilika baada ya usawa.
Kwa maneno mengine, kama bei zilikuwa na muanguko wa soko kwa muda mrefu, muda si mrefu itaanza kupanda. Hakuna chaguzi nyingine.
Baada ya kuwa katika soko linaloshuka, zinakuwa nafuu na kuwavutia wanunuzi, tangu sasa fedha kidogo itahitajika kuzinunua. Wakati huohuo, zinapoendelea kushuka zaidi, ndivyo nguvu kubwa kwa ukuaji wa baadaye. Hivyo sheria ya kwanza — “nunua chini”.
Mazingira mengine ni kama ifuatavyo: wakati hisa za eBay zinakuwa kwa kuda mrefu, muda si mrefu au wakati mfupi ujao utakuja wakati wanunuzi wakubwa watafikia malengo yao na kuchukua faida.
Wakati hili linatokea, usambazaji wa fedha ambao ulichangia ukuaji utaondoka, na usambazaji wa fedha kwa wale walioamua kucheza na uuzaji wa muda mfupi wa CFD utabaki katika mali. Na ndipo uzambazaji wa fedha za wauzaji utazidi ukubwa wa wanunuzi, kugeuka na kushuka kwa hisa huanza. Hivyo sheria ya pili — “uza juu”.
Nadhani hakuna ugumu katika mbinu hii. Kila mmoja anaijua, na hii inafanya kazi vizuri. Imefanya kazi miaka 100 iliyopita na inafanya hata sasa.
Biashara ya CFD kwa Kiinua Mtaji
Kuna sehemu nyingine ya muhimu katika biashara. Sasa ni wakati wa kuzungumzia kiinua mtaji. Kiinua mtaji katika Forex ni mkopo usio na riba unaotolewa na wakala, ambao unakuwezesha kufanya biashara kwa ujazo mkubwa kuliko mtaji wako.
Bila ya kiinua mtaji ambacho wakala anakitoa, biashara katika mabadilishano kwa watu binafsi isingekuwa na faida kwa mfanyabiashara na wakala. Hata hivyo, ni muhimu kufahamu kuwa inawezekana kupoteza fedha wakati wa kufanya biashara ya CFD bila ya kiinua mtaji. Ni chombo cha mtego, kwa upande mmoja inakusaidia kuongeza kipato, lakini, kwa upande mwingine, inaweza kufanya akaunti yako ya uwekezaji kupoteza fedha.
Mbali na sababu kwamba mabadilishano ya hisa ya dunia yanafanya kazi, mabadiliko ya kila siku ya bei ni kama thamani ya asilimia moja ya mali husika. Na bila ya kiinua mtaji, kipato cha mfanyabiashara kinaweza kuwa senti chache hata kwa biashara zenye mafanikio.
Kwa mfano, unataka kununua hisa 1 ya Hewlett-Packard, inayogharimu $18. Hata katika siku njema, thamani ya hisa inaweza kubadilika kwa dola 3-4, na hivyo kipato chako kitakuwa dola 3. Unatengenezaje mamilioni katika mabadilishano? Unaweza kufanya hivyo kwa kiinua mtaji.
Tuangalie mifano:
Mfano wa 1
Kwanza, tuangalie kiinua mtaji kwa sarafu.
Tuseme tumeamua kutengeneza fedha katika mabadiliko ya viwango vya jozi za sarafu. Kwa mfano, tutachukua jozi ya sarafu ya USDCHF, iliyokuwa 1.0000 muda si mrefu.
Tumeamua kuwa kiwango cha sarafu kitapanda, na hivyo tunahitaji kununua.
Ukubwa wa msingi wa mkataba kwa sarafu ni vipande 100,000. Kwa maneno mengine, biashara ya loti 1 ya CFD itatengeneza kipato au hasara kama kutokea kwenye $100,000. Ili kuepuka hasara kubwa kama ikishindikana, inaweza kupunguzwa kwa kiwango kidogo cha loti 0.01, na kisha ujazo wa sarafu utakuwa 1,000.
Tunanunua loti 0.01 ya jozi ya sarafu ya USDCHF ikiwa 1.00000 tukitumaini ipande. Kwa suala hili, kila alama ya mwendo wa muda mfupi wa juu au wa chini italeta faida au hasara, kutegemea na loti yetu. Kwa loti ya 0.01, kila alama itakuwa sawa na $0.01.
Baada ya muda bei ilipanda na nukuu ilikuwa 1.01000. Iliongezeka kwa alama 1,000. Kwa hiyo faida kwa biashara yetu ya CFD itakuwa 1,000 * 0.01 = dola 10.
Kama tukitumia ujazo mkubwa, kwa mfano 0.1, basi faida itaongezeka mara 10 na kuwa $100, na kuendelea. Kadiri kiinua mtaji kinavyokuwa kikubwa, ndivyo uwezekano wa faida utakavyokuwa, lakini usisahau kuhusu hatari kubwa na uwezekano wa mwito wa mtaji. Kwa suala hili, hasara yako itaongezwa na kumaliza amana yako kwa haraka.
Mfano wa 2
Sasa tuangalie namna kiinua mtaji kinavyofanya kazi kwa suala ya mikataba kwa tofauti.
Tuchambue namna kiinua mtaji kinavyofanya kazi kwa hisa za Google. Wakati wa kufanya biashara CFD, ujazo wa chini mara nyingi ni hisa moja, kwa maneno mengine loti 1 ni sawa na hisa 1.
Hisa moja inagharimu $1,444, na kwa suala la soko la Forex, hatuhitaji kiwango chote katika salio. Lakini zaidi katika hilo baadaye.
Wakati wa kununua hisa 1, kiinua mtaji kitakuwa 1:1 na kitaratibiwa na ongezeko rahisi katika namba za hisa zilizonunuliwa.
Kama tunanunua hisa 10, kiinua mtaji kitakuwa 1:10. Kama tutanunua hisa 100, kiinua mtaji kitakuwa 1:100. Haitakuwa rahisi.
Bei ya alama moja kwa loti 1 mara zote itakuwa sawa na mabadiliko madogo katika bei ya hisa, ambayo ni senti 1 au dola 0.01.
Tufanye mahesabu kiasi gani tutatengeneza kama hisa itapanda kutoka $1,444 mpaka $1,450.
Kama tunanunua mkataba 1, faida itakuwa sawa na idadi ya alama zilizopita zikizidishwa kwa bei ya alama, au 600 * 0.01 = $6.
Basi, kwa uhakika, kama ukiongeza kiinua mtaji, unahitaji kununua mikataba zaidi, kwa mfano, 100, kisha faida itaongezeka mara 100 na kiwango kuwa dola 600.
Mtaji katika biashara ya CFD
Bila ya kiinua mtaji ambacho wakala anakupatia, biashara katika mabadilishano haingewezekana kwa watu binafsi, na kipato cha wakala kingekuwa karibu na sifuri.
Hivyo biashara ya mtaji ni nzuri kwa kila mtu anayehusika katika hatua ya biashara. Kwa msaada wa mtaji, wafanyabiashara wazoefu wanaweza kufanya miamala ambayo kwa mitaji yao wenyewe isingetosha. Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kuhusu mahitaji ya mtaji kuepuka uwezekano wa mwito wa mtaji.
Kwa mfano, unataka kununua hisa 10 za Google. Si kila mtu ataweza kumudu, tangu hisa moja inagharimu $1,445, na kumi — $14,450. Kwa msasada wa uazimaji wa mtaji, ninaweza kununua hisa 100 za Google kwa upekee wa $400 katika akaunti yangu ya mfanyabiashara ya CFD.
Tuangalie mfano:
Juu, nimekupatia fomula ya kuhesabu mtaji. Hii hapa tena:
Kigezo muhimu ni asilimia ya mtaji, inaelezea thamani ya jumla ya mali unayohitaji kuwa nayo katika akaunti yako kukamilisha biashara hii.
Kwa mfano, kwa suala ya hisa za Google, mtaji ni 2% pekee ya thamani nzima. Kwa maneno mengine, kununua hisa 1 tunahitaji $28.89 pekee badala ya $1,444. Shukrani kwa hili, tunaweza kumudu zaidi ya hisa 30 kwa $1000 pekee katika akauti yetu.
Biashara ya pande mbili ya CFD
Sasa ninataka kukuambia kuhusu mbinu inayotegemewa kwa biashara ya CFD. Hii ni mbinu ya pande mbili. Katika ulimwengu wa fedha, biashara ya pande mbili ni njia ya kulinda kipato kutoka kwenye hatari ya kupoteza mtaji. Kwa suala letu, tutatumia biashara ya pande mbili dhidi ya hatari kubwa inayowezekana ya masoko yanayoshuka.
Picha ya juu inaonesha namna inavyofanya kazi.
Kwa mfano, tumeamua kununua hisa ya Apple. Soko linapanda kwenye chati na kila kitu kinaonekana kipo sawa. Lakini ghafla tunajifunza kuwa kampuni inaweza kuwa na matatizo ya muda mfupi ambayo yanaweza kuhusiana na toleo bovu za iPhone mpya. Hili halijaathiri soko bado, lakini inategemewa kwa ukubwa kuwa itaathiri.
Hakuna maana yoyote ya kufunga biashara, kwa kuwa tatizo ni la muda mfupi na bei inapaswa kupanda kwa kipindi kirefu. Kwa suala hili, kuna ujanja tunaweza kufanya. Tunakwenda kwenye akaunti ya pili na kufuatilia mienendo ya bei ya chati.
Baada ya muda, hisa imeanza kushuka kweli, na kwa muda ambao bei imefika usawa wetu cha kununua, tunafungua nafasi nyigine inayofanana katika akaunti ya pili (kwa ujazo unaofanana), lakini muda huu ni nafasi ya kuuza.
Kama bei itashuka chini zaidi, faida itaanza kutengenezwa katika akaunti ya pili, ambayo itakuwa sawa na hasara ya kwenye akaunti ya kwanza.
Baada ya kusubiri kwa muda, tuna uamuzi. Tunaweza kufunga nafasi ya faida katika akaunti ya pili na kuzubiri bei ipande na kurudi kwenye faida katika akaunti kuu. Au tunaweza kusubiri mpaka bei irudi kwenye usawa ambao tulianzia.
Hapa uamuzi ni wako, lakini unahitaji kuelewa ni kwa nini unafanya muingiliano huu. Kama unataka kupata faida za ziada, una chaguo la 1, lakini ni hatari. Kama unataka kuepuka hasara ya uda mfupi, una chaguzi ya 2, linaloitwa kuvunja kwa usawa.
Mbinu za Biashara ya CFD kwa Wataalamu
Sasa tuongelee namna biashara ya CFD inavyofanya kazi kwa wafanyabiashara wazoefu. Hii haimaanishi kuwa haifai kwa wanaoanza, wanahitaji kiwango fulani cha maarifa. Daima kuna mfumo wa mkakati wa uchambuzi wa msingi wa kiufundi na mkataba kwa muundo tofauti.
Tuanze na iliyo maarufu zaidi.
Biashara ya Mipakani (Range)
Labda mbiinu ya masafa ni maarufu zaidi baia ya wafanyabiashara wa Forex.
Sheria ya muhimu ya mbinu inahusu mifereji ya bei. Unafuatilia mienendo ya chati kwa mabadiliko ya upandeupande au ya ukanda yenye mlalo wa wastani. Kisha unaongeza moja ya viashiria vya mfereji (CCI au RSI) na kulinganisha juu na chini katika mfereji wa bei zenye alama ambazo mstari wa kiashiria unavuka ukanda wa kununuliwa sana na kuuzwa sana.
Kama alama zinagongana kabisa, hii ni ishara ya kuingia kwenye soko. Kama bei imefikia mstari katika chati, lakini mstari wa EMA haujafika kwenye ukanda wa kiashiria, ishara kama hiyo haijitoshelezi na haichukuliwi katika matumizi ya mbinu hii.I
Mivunjo
Mbinu ya mivunjo pia ni maarufu kwa wafanyabiashara.
Inatumika zaidi katika vipindi vya ndani ya siku.
Kama ilivyokuwa katika mbinu iliyopita, inatokana na kuvunjwa kwa mienendo ya upandeupande au usawa. Mistari ya Bollinger na maumbo ya Bill Williams ractals yanatumika kama viashiria.
Unaangalia kwa muda katika chati wakati bei inavunja usawa wa umbo lililo karibu na unasubiri chati iende zaidi ya mpaka wa mstari wa karibu zaidi wa Bollonger. Kisha ishara inahesabika kuwa ya kweli. Kizuia hasara kinawekwa daima katika usawa wa umbo linalokinzana.
Uwekezaji wa kinyume
Mbinu ya uwekezaji wa kinyume ni zaidi ya mbinu ya msingi, kwani inahusika sio tu na chati ya bei, bali na usomaji wa maoni ya umati wa watu.
Mbinu hii ilielezewa kwanza na Benjamin Graham ikwenye kitabu chake cha The Intelligent Investor, ambapo alifananisha maoni ya watu na machafuko yaliyodhibitiwa.
Msingi wa kanuni ni kutafuta alama za kupinga uelekeo. Unaweza kutafuta mali ambayo ina msukumo wa uelekeo uliosemwa na kutengengeza nafasi ya kupinga mwenendo huo.
Kwa maneno mengine, unafanya biashara kupingana na maoni ya soko. Hisa za Tesla zinaweza kutumika kama mfano. Wakati ilipotangazwa wiki iliyopita kuwa kampuni haitahusika katika fahirisi za hiza za S&P500, wavivu pekee hawakuuza. Hii ni hali halisi kwa mbinu hii. Kuna uwezekano mkubwa wa kugeuka na kukua katika wakati mfupi ujao.
Kufuata Uelekeo
Mbinu ya kufuata uelekeo ni maarufu baina ya mbinu za kiashiria. Hata hivyo, kwa maoni yangu, ina kiwango cha hasara kulinganisha na mbinu ya mfereji.
Msingi ni kufungua nafasi katika uelekeo wa uelekeo mpya uliotengenezwa. Unapata alama za muundo wa uelekeo unaotokana na ishara kuu kutoka kwenye maingiliano ya mistari ya wastani wa kuelekea wa haraka (vipimo 21) na wa taratibu (vipimo 55). Kisha ishara inachujwa kwa kutumia mistari inayorudiarudia mara nyingi MACD na RSI. Hakikisha kuwa bei inabaki ndani ya ukanda wa RSI, na bei katika uelekeo unaotakiwa katika MACD.
Kwa mfano, katika suala hili la nafasi ya kununua, EMA ya haraka imekutana na ya taratibu katika chati na kwa wakati mmoja, RSI ndani ya mfereji, na viboksi vya MACD ni vya ueleko wa juu — ishara ni ya kweli, unaweza kununua. Biashara inapaswa kufungwa wakati kiashiria cha RSI kikivuka mfereji.
Kukatakata (ama Biashara ya Tofauti kwa Bei)
Kuna mbinu za kukata kata nyingi, lakini nitashauri uhusishe kiashiria cha kipindi cha kukatakata, ambacho kinafaa kufanyia biashara CFD.
Mbinu hii inahusiana na kulinganisha ishara kutoka kwenye viashiria vikubwa vinne 4. Ishara kuu ni kutoka kwenye bembea za MACD, na kisha tunaangalia ishara hii kwa kutumia RSI na MA mbili.
Maana ya mbinu hii ni kuwa ishara inaendana katika viashiria vyote vinne.T
Mfano wao upo katika chati juu.
Tunapata ishara ya kununua wakati: MACD inatengeneza baa ya kwanza juu ya usawa wa 0, RSi inapita katikati ya usawa wa 50 kwenda juu, na mstari wa umiano wa haraka uliolala wenye kipindi namba 10 upo juu ya mstari wa uwiano wa kielelezo wenye kipindi namba 26.
Biashara ya Kubembea
Mbinu ya kubembea sio mbinu, tofauti na watu wanavyodhani. Biashara ya Kubembea ni sheria tata jumuishi, njia na elimu ya soko pamoja ambayo inakupa mpango wa wazi na wenye muundo unaohusika na kila taarifa kwa undani.
Kwa ujumla, biashara ya kubembea inahesabika kuwa njia ya biashara ambayo mfanyabiashara anatunza nafasi kufuata uelekeo kwa muda mrefu kadiri inavyowezekana, akipuuza mwendo wa urekebishaji. Kwa mtazamo mzuri, hii huleta faida sio kwa kipande kidogo, bali kwa uelekeo mzima.
Nafasi za kubembea mara nyingi zinatunzwa kwa kwa zaidi ya mwezi. Lakini kuna nafasi za kubembea za jumla.
Katika chati hapo juu unaweza kuona biashara yangu halisi ya dhahabu, ambayo nimeiacha wazi kwa karibu mwaka, kwa kuongeza na kupunguza biashara za muda mfupi zinazohusiana nayo bila ya kugusa nafasi kuu.
Kwa ujumla, ninaiona biashara ya kubembea kuwa kilele cha sanaa ya biashara, na ninakwenda kuandika makala tofauti kuhusu njia hii hivi karibuni.
Kucheza na Habari
Biashara ya Habari ni njia maarufu ya biashara.
Kama ilivyo sheria, biashara ya habari imegawanyika katika aina 2: biashara ya habari za vipindi na biashara ya matukio. Biashara ya vipindi inafanya zaidi kwa kutumia kalenda ya kiuchumi. Lakini kwa biashara ya matukio, unahitaji kufahamu kila kitu ambacho kinatokea kuzunguka zana unayoipenda.
Kw mfano, nimechagua matukio yanayohusu Walmart Inc. Mwishoni mwa mwezi wa Agosti, ilitangazwa kuwa kampuni ilinunua huduma maarufu ya TikTok na hisa zikaanza kupanda sana. Huu ni mfano wa biashara ya kununua. Hata hivyo, mwenzi mmoja baadaye, habari ilionekana katika vyombo vya habari kuwa serikali ya China ingeweza kuzuia biashara hii, na bei ya hisa ya Wal-Mart ilianza kushuka kwa kasi — hii ni ishara ya kuuza.
Faida & Hatari za CFD
Kwa hiyo biashara ya CFD ni nini na nini cha muhimu katika biashara ya CFD? Njia ya kutengeneza fedha au zana nyingine ya kiuchumi isiyo na umuhimu?
Uchambuzi wa faida na hasara utakusaidia kujibu swali hili.
Wakati mawakala duniani wameanza kufanya biashara ya mikataba ya tofauti miaka kumi iliyopita, kwa hakika, nilijiuliza: “CFD ni nini hasa?”
Kama nilivyosoma aina mpya za mikataba, nimefahamu idadi ya faida zake juu ya mikataba iliyopo. Hata hivyo, muda unavyozidi kwenda, nimefahamu hasara pia. Tuziangalie zote.
Faida za CFD
Nimekuwa nikifanyia mazoezi biashara ya CFD. Hii imenisaidia kugundua faida kuu nne juu ya aina nyingine za mikataba:
Unahitaji mtaji mdogo kufanya biashara. Nimeongelea kuhusu faida hii mara nyingi katika makala hii.
Mtaji ni faida kubwa inayofanya CFD ifanye kazi karibu kwa kila mtu. Mtaji wa 2% ni nini ukilinganisha na bei ya hisa ya $1,500? Kwa dola 30, nimepata fursa ya kupata 100, 200,300 na hata kipato cha dola zaidi kwa siku.
Kamisheni za chini kabisa. Inapokuja kwenye kununua hisa za kampuni kwa muda mrefu, kwa kipindi cha miezi kadhaa mpaka mwaka mmoja, Ninafikiria kuhusu ada.
Ada hizi zinahusisha kodi, kamisheni kwa ujumla katika usajili wa wanahisa, uwezekano wa kuwekwa kwa kamisheni (kwa suala la bidhaa), kiinua mtaji, gharama za kupitisha siku na nyinginezo.
Mkusanyiko huu unanifanya nifikirie kwa umakini kabla ya kununua zana yoyote kwa mtaji wako ulionao.Hata hivyo wakati ninaamua kununua CFD, siufikirii kabisa, kwa sababu ninacholipa ni tofauti ya bei kwa mara moja, kamisheni ya senti 25 kwa loti, na makato ya kulaza biashara, ambayo ni pungufu ya senti moja.
Kwa mfano, wakati wa kununua mkataba wa hisa 1 ya Google, utalipa senti 80 katika tofauti ya bei, senti 25 ya kamisheni na senti 1 kwa siku kumi za umiliki. Ni hivyo tu! Kwa mkataba wa $1,500, unalipa $1 ya kamisheni. Hitimisho ni dhahiri.
Chaguzi ya biashara pande mbili. Nimeshaongelea kuhusu biashara ya pande mbili hapo juu. Kuna dhamana nyingi za hisa kwa ajili ya biashara kinzani, kama chaguzi na zijazo, lakini mikataba ya tofauti ni nafuu zaidi kulinganisha na hizo.
Kwa kweli, mikataba ya tofauti ni njia sahihi ya kuunda nafasi za kufunga na kusanidiwa. Lakini faida yao kubwa ni uwezo wa kufanya biashara kinzani ya muda mrefu katika hisa halisi. Nimeielezea hatua hapo juu.
Urahisi. Kipengele hiki kinatoa muhtasari wa yote hapo juu. Urahisi unatumika kwenye kila kitu kinachohusiana na mikataba ya tofauti. Mtaji wa chini, na kiinua mtaji kisicho na kikomo, na kwa utendaji hakuna kamisheni. Lakini faida moja inatajwa kwa upekee — upatikanaji.
Mawakala wa Forex wanatoa biashara ya CFD kwa aina zote za zana katika kituo kimoja rahisi. Huhitaji kuwa na akaunti tofauti katika mabadilishano, watoa huduma wengi wa CFD wana ufikiaji wa aina zote za mikataba maarufu ya tofauti.
Hatari za CFD
Kwa hasara, nimezipata mbili tu. Labda sio hasara hasa, lakini, ninapendekeza uwe makini kwa vitu vidogo, kwa sababu vinaathiri matokeo.
Hakuna uendeshaji wa kisheria.
Nafikiri wengi wanaweza kusema, “Tunazungumzia aina gani za sheria kama tunafanya biashara na majukwaa ya biashara ya nje na hatulipi kodi?”
Hii ni kweli, na ninafurahi kuwa sihitaji kulipa kodi. Lakini nitakupa takwimu zifuatazo.
Katika miaka ya hivi karibuni, kesi nyingi za madai baina ya mawakala na wateja wao wa rejareja zinazohusu zaidi biashara za CFD zimekuwa nyingi. Hii ni kwa kwa sababu wakala mara nyingi ni muongozaji wa soko la mikataba kwa tofauti, hivyo wamejiwekea taratibu zao binafsi. Hakuna taarifa za za maandishi za CFD na hii inafanya kutokuwa na viwango. Kwa suala lolote la madai, wakala daima atakuwa na haki.
Kwa sababu hii, ninapendekeza sana kufanya biashara ya CFD kupitia wakala aliyethibitishwa. Ni vizuri kuchagua mtoa huduma wa CFD mwenye kamisheni ya juu kidogo ili uwe na uhakika kwamba hujadanganywa.
Mwekezaji wa CDF sio mmiliki wa hisa.
Tena tunaweza kusema hii sio kama hasara.
Hii inaweza isiwe muhimu kwa wanaoanza, lakini ni tofauti kwa mfanyabiashara mzoefu.
Tofauti kati ya kununua nafasi ya CFD na kununua hisa inayoonekana upo kwenye kanuni.
Kama umenunua hisa na umeingia katika usajili wa mmiliki hisa, utakuwa mmiliki wake mpaka pake utakapoiuza au kuihamisha kwa mtu mwingine. Hakuna kitu kingine, iwe mafuriko, moto, migogoro ya dunia, mlipuko wa COVID-19, kufilisika kwa wakala wako au kitu kingine chochote, kinaweza kuathiri mfumo huu kwa njia yoyote. Hisa itabaki kuwa yako hata kama wakala ambaye kupitia yeye umeinunua na haijawahi kuwa wakala kwa miaka 10.
Hata kama kampuni ambayo hisa yake umeamua kuiuza au kampuni nyingine ikainunua, bado utakuwa na hisa na itakuwa na thamani.
Wakati wa kazi ya kuendesha hisa, wakala wako pekee atakuwa anahusika nayo. Kama kitu kikitokea, mikataba yako itapotea kama tu ilivyojitokeza.
Kwa hiyo, mara nyingine tena — chagua mawakala wanaoaminika!
Majukwaa ya Biashara ya CFD & Zana
Sasa ni wakati wa kuongelea kuhusu zana za kiuchumi unazotumia wakati wa kufanya biashara ya CFD.
1. Majukwaa ya Biashara
Mikataba ya Tofauti ni mikataba inayofanyiwa biashara ya mabadilishano zaidi, na kwa hiyo haihitaji programu ya upekee. Kituo cha kawaida cha biashara kinachotolewa na wakala wako kinatosha kuendesha kazi ya CFD.
Jukwaa maarufu zaidi, kwa hakika, ni kituo cha biashara cha MetaTrader 4. Kwa maoni yangu, hakuna kituo bora zaidi cha biashara. Kina kila kitu unachohitaji kwa ajili ya biashara, na uwezo wa kupakua historia ya chati.
Kuna toleo jingine jipya la kituo hiki, MT5, lakini si maarufu kama MT4.
Kuna majukwaa kadhaa marahisi ya mtandaoni ambayo yameanza kuonekana. Faida yake ni urahisi, tangu jukwaa limejengwa katika akaunti binafsi ya mfanyabiashara, na mmiliki anaweza kufikia kwa upesi fursa zote za kuhusiana na wakala.
2. Zana za Biashara
Zana ni vitu vyote vya ziada ambavyo wakala wako anakupatia.
Hii inahusisha kalenda za kiuchumi na ufikiaji wa bure wa uchambuzi wa muhimu. Watoa huduma wanaotegemewa pekee wanaweza kukuhakikishia hili kwani si kila mtu anaweza kumudu idara yake mwenyewe ya uchambuzi. Kuna programu za ziada, zikihusisha kikokotoo cha mfanyabiashara ambacho nimeshakielezea. Unaweza pia kuongeza mipasho ya habari, ambayo ni muhimu kwa wafanyabiashara wa habari.
3. Vipengele vya uchambuzi wa picha
Zana hizi mara nyingi zinajengwa ndani ya jukwaa la biashara. Lakini muda muda hausimami na viashiria vipya vya biashara au vipengele vya picha vinaonekana daima. Unahitaji kupakua, kusasisha, na kuzifanyia mazoezi ya biashara katika kituo cha biashara.
4. Washauri wa biashara
Zana hizi ni muhimu kuendesha biashara yako kiotomatiki. Kufanya biashara kwa roboti za biashara kunaitwa biashara ya algorithmic. Faida yake ni kwamba zinafanya kazi nyingi za mfanyabiashara, kuanzia kwenye kutafuta ishara za kuingia sokoni, mpaka kwenye biashara kamili ya kiotomatiki bila ya ushiriki wa mfanyabiashara.
Mfanyabiashara mwenye mafanikio ana jumla ya zana zote katika ghala yake. Mawakala wanaoongoza wanatambua hili na wanajaribu kuwapa wateja wao jumla hii katika sehemu moja na jukwaa moja.
Nimesema zaidi ya mara moja, nimechagua LiteFinance — wakala mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 15 katika masoko ya fedha.
Nimefanya kazi na wakala huyu kwa zaidi ya miaka 5, baada ya kujaribu mawakala mbalimbali kabla ya hapo.
Faida kuu ya LiteFinance ni ufikiaji wake.
Kila kitu unachohitaji kipo ndani ya sehemu moja.
Muundo wa tovuti ni rafiki kwa mtumiaji — huhitaji kupita kwenye viungo vingi kwenda unapotaka. Unapata kila kitu katika mibofyo 2 au 3.
Kama mtaalamu, ninaridhika kabisa na masharti ya biashara, kamisheni, na uitikiaji wa seva katika mabadiliko ya papo kwa hapo ya bei au mitelezo. Pia, kampuni inaruhusu biashara ya kukatakata na kubembea.
Sheria & Dondoo za CFD
Sasa nakupatia baadhi ya dondoo kwa kujenga mbinu yako ya mafanikio ya biashara. Haijalishi itasikika namna gani, kila mbinu ni mkusanyiko wa sheria, tutengeneze sheria:
1. Daima fuata sheria!
Sheria ya kwanza na yenye kipaombele ni daima kufuata mbinu yako ya biashara. Makosa yoyote au kuendekeza kunaweza kupelekea hasara au matatizo.
2. Tumia maagizo ya zuio
Wakati wa kufanya biashara ya CFD, utahusika na hisa zaidi, na biashara ya hisa ina muda wake. Kutakuwa na mapumziko katika biashara, baada ya mabadiliko yasiyotarajiwa kutokea. Kuzuia mabadiliko haya kuathiri pochi yako, unapaswa muda wote kuzuia hatari.
3. Usiogope kufanya maamuzi
Nafahamu kutoka kwenye uzoefu wangu kwamba hautaunda mbinu ya uwekezaji yenye mafanikio kama utaogopa kufanya makosa. Bila ya makosa, hautajifunza. Kuepuka makosa makubwa, angalia pointi ya 2.
4. Angalia kiinua mtaji chako
Mara zote angalia kiinua mteja katika uwanda uliopangwa kabla ya kufungua biashara na usifanye chochote ambacho hujakipanga awali.
Kwa maneno mengine, kama upo kwenye biashara, na tukio limetokea kuthibitisha utabiri wako, haupaswi kuongeza nafasi kama hukupanga hivyo kabla.
5. Fanya mahesabu ya biashara yako kabla ya kuifungua
Kabla ya kufungua biashara, unapaswa kufahamu wazi una lengo gani na kiasi gani utapoteza kama haitaenda sawa.
6. Usimsikilize mtu
Kama mtu atakuambia kuwa amepata mamilioni katika Bitcoin, haimaanishi kuwa unapaswa kuacha kila kitu na kununua Bitcoin. Kumbuka, uvumi mwingi unaundwa kwa malengo, na hautaleta faida yoyote. Kama mtu atakuambia kuwa LiteFinance ni wakala mzuri na wa kuaminika, usimuamini bila kuona – fanya tafiti yako na ufanye hitimisho lako.
7. Tumia mapumziko ya biashara
Haupaswi kuwa katika soko muda wote. Chukua mapumziko, mwili wako unayahitaji. Uchovu hupelekea makosa. Inasaida kuchukua mapumziko baada ya biashara mbaya.
8. Chambua makosa yako
Kuzuia hatari ya upoteaji wa haraka wa fedha, baada ya kufanya biashara mbaya, amua kama yalikuwa makosa yako au ni hatari za soko zisizo na maana. Kama kulikuwa na makosa ya soko na umefunga biashara katika hasara, lakini ndani ya sheria zako mwenyewe, jipongeze, kwa sababu hata katika hali ngumu umebaki kuwa mkweli kwa mbinu yako.
Makosa ya soko hayatokei sana, na kama ukiwa tayari kwa ajili yake, faida yako itakuwa.
Biashara ya CFD vs. zana nyingine za fedha
Kilichobaki ni kufananisha CFD na zana nyingine zinazotolewa na makampuni na mawakala.
CFD vs. Biashara ya Gawio (Hisa)
Wakati wa kufananisha hisa za CFD na hisa halisi, kuna vitu vingi vinapaswa kutajwa:
Faida za CFD:
- Mahitaji ya Kiwango cha chini cha mtaji;
- Kiinua mtaji kisicho na kikomo;
- Hakuna kamisheni na kodi;
- Uwezo wa kufungua mauzo ya muda mfupi ya CFD;
- Uwezekano wa biashara kinzani.
Faida ya soko halisi la hisa
- Miamala inaendeshwa na sheria;
- Inaweza kuwa mali ya dhamana katika migogoro ya kiuchumi;
- Katika suala la mtaji mkubwa wa wakama, hisa itabaki;
- Mmiliki ni mwana hisa anayepiga kura kwenye kampuni.
CFD vs. Bashiri za Tofauti ya bei
Wakati wa kufananisha CFD na bashiri za tofauti ya bei, kuna vitu vingi ambavyo vinapaswa kutajwa:
Faida za CFD:
- Mahitaji madogo ya mtaji;
- Kiinua mtaji kisicho na kikomo;
- Hakuna kamisheni na kodi;
- Inaendeshwa na sheria “kwa shughuli ya muuzaji”;
- Uwezekano wa biashara kinzani.
Faida za bashiri za tofauti kwa bei:
- Mteja anaweka ukubwa wa biashara;
- Uwezo wa kufanya biashara ya tofauti kwa bei.
Hasara za bashiri ya tofauti kwa bei:
- Hakuna mfumo wa uendeshaji;
- Shughuli zinazolingana na uwekaji vitabu;
- Vizingiti vya juu vya faida.
CFD Vs. Zijazo
Wakati wa kufananisha biashara ya CFD na ununuaji wa mikataba ya zijazo, kuna vitu vingi ambavyo vinapaswa kutajwa:
Faida za mikataba kwa tofauti:
- Mahitaji madogo ya mtaji;
- Kiinua mtaji kisicho na kikomo;
- Hakuna kamisheni na kodi;
- Uwezo wa kufungua mikataba ya kuuza;
- Uwezo wa biashara kinzani;
- Mitaji mikubwa sokoni;
- Mkataba hauna kikomo cha muda.
Faida za Mikataba ya Zijazo:
- Uwezekano wa kufanya biashara kinzani kwa mali husika;
- Uendeshaji wa kisheria;
- Uwezo wa kufungua mikataba ya kuuza;
- Uhakikisho wa utimilifu wa majukumu chini ya mkataba.
CFD vs. Chaguzi
Wakati wa kufananisha biashara ya CFD yenye mikataba ya kununua ya chaguzi, kuna vitu vingi vinapaswa kutajwa:
Kwanza nitasema, kama hakuna kusingekuwa na CFD, ningeziita chaguzi kuwa zana bora za fedha katika historia bila ya kusita.
Faida za mikataba kwa tofauti:
- Kiwango kidogo cha mtaji;
- Kiinua mtaji kisicho na kikomo;
- Hakuna kamisheni na kodi;
- Uwezo wa kufungua mikataba ya kuuza;
- Uwezo wa kufanya biashara kinzani;
- Mitaji mikubwa;
- Mikataba haina kikomo cha muda.
Faida za Mikataba ya Chaguzi:
- Uwezekano wa biashara kinzani nafuu kwa mali husika;
- Uendeshaji wa kisheria;
- Uwezo wa kuuza na na kununua mkataba;
- Uhakikisho wa utimilifu wa majukumu chini ya mkataba;
- Mfumo bora uliojengwa wa kuzuia hasara kwa zana zote za mabadilishano.
Hasara za Mikataba ya Chaguzi:
- Mtaji mdogo;
- Tafadhali tambua! Chaguzi za Binary ni kivuli cha soko lisiloratibiwa la OTC. Kuna uwezekano mkubwa wa kukutana na watoa huduma za fedha matapeli.
Hitimisho
Kwa majumuisho, ninapenda kusema kuwa biashara ya CFD ni chaguzi la pekee kwa wanaoanza na wafanyabiashara bila ya mtaji wa msingi. Wafanyabiashara wenye kiwango kikubwa cha fedha katika ugawanyaji huu wa mtaji wanaweza kuchagua kununua mali husika yenyewe kulingana na uendeshaji usiokidhi wa kisheria na hatari kubwa ya kupoteza fedha kwa matumizi ya kiinua mtaji.
Wakati wa kufanya maamuzi ya mikataba kwa tofauti, ni muhimu kukumbuka hatari zinazohusiana na mikataba ya CFD. Bila ya mpango mzuri wa kuhimili hatari, akaunti za wafanyabiashara wa rejareja wa CFD zinaweza kupoteza mtaji kwa haraka. Kama umeamua kuchagua ada ndogo na gharama ndogo, basi CFD wanatoa chaguzi zuri kwa njia nyingine za biashara.
Hata, kumbuka kuwa kipimo kikuu cha mafanikio kwa mfanyabiashara yoyote ni kiwango cha faida, chaguzi ya zana haihusiani sana.
Majadiliano yametosha, ni muda wa kufanya kazi. Nakutakia kila jema. Kama una maswali yoyote, nina furaha kukusaidia!
FAQ za Biashara ya CFD
CFD au mkataba kwa tofauti ni makubaliano maalumu baina ya sehemu mbili (muuzaji na mnunuzi) kuhamisha tofauti baina ya bei iliyofikiwa ya mali husika wakati wa kufungua biashara na thamani yake wakati wa kufunga biashara. CFD ni zana tata ambazo hazishauriwi kwa wanaoanza. Wawekezaji wanapaswa daima kuwa makini kwamba biashara ya CFD inahusisha hatari na hakuna dhamana ya mafanikio. Kuzuia akaunti yako kwenye kupoteza fedha kwa haraka, ni muhimu kuendelea kujifunza mwenyewe na kufanya mazoezi ya biashara ya zana hii tata.
Biashara ya CFD ni njia ya kuingia kwenye miamala katika mabadilishano kwa kutumia chombo cha dhamana ya fedha. Wafanyabiashara wa CFD wanakamilisha mikataba ya tofauti kwa bei nzuri ya mali husika. Mali inaweza kuwa hisa, bidhaa, sarafu, au fahirisi ya hisa za CFD. Mkataba hautoi umiliki halisi wa mali husika. Ni muhimu kukumbuka kuwa biashara nyingi ca CFD inahusisha hatari kubwa ya kupoteza fedha, ana hivyo ni muhimu kuongeza maarifa katika eneo hili na kufanya mazoezi ya biashara kwa zana hizi tata.
CFD katika Forex inatoa ufikiaji wa mikataba ta tofauti bila ya kusajili akaunti ya biashara katika baadhi ya mabadilishano. Mawakala wa Forex wanatoa fursa kufanya biashara katika zana mbalimbali kwa kutumia akaunti moja ya biashara.
CFD ni zana tata ambazo zinatumika kama njia ya kupita vikwazo vya kisheria vinavyozuia wananchi wa nchi mbalimbali kufanya miamala kwa dhamana za mamlaka nyingine za fedha. Pia, mikataba ya tofauti ni njia nafuu ya kununua hisa za makampuni ambazo mwekezaji hana fedha za kutosha kuzinunua. Hata hivyo, tambua kuwa CFD ni aina ya hatari ya uwekezaji na bila ya ujuzi wa muhimu na uzoefu inaweza kufanya akaunti yako ya uwekezaji wa rrejareja kupoteza fedha haraka.
Ndio.CFD hutumia mfumo wa kawaida wa ujazo wa “loti”. Kiwango cha chini kabisa cha loti kwa hisa ya CFD kawaida ni 1, ambayo ni sawa na hisa moja. Katika aina hii ya muamala, kiinua mtaji chako kitakuwa 1:1. Biashara kwa kutumia kiinua mtaji chako huwa na hatari nyingi, hivyo haipaswi kufanyika kwa uzembe. Wafanyabiashara wa CFD wana uwezo wa kupata fedha nyingi kwa haraka lakini pia hukabiliwa na uwezo wa kupoteza fedha nyingi kutokana na kiinua mtaji pamoja na kukosa uzoefu. Ni muhimu kila wakati kutambua hatari zinazohusiana na biashara hizi na kuhakikisha kuwa akaunti zako za uwekezaji hazipotezi pesa pindi ufanyapo biashara kwa kiinua mtaji.
Kufanya biashara ya pande mbili katika mali halisi kwa kutumia mikataba kwa tofauti, unahitaji kufungua biashara ya CFD katika mali hiyo kwa uelekeo tofauti kwa mali husika. Kama umenunua mali husika, unahitaji kufungua nafasi ya chini na CFD kwa ujazo unaofanana. Kama umeuza mali husika, biashara ya CFD inapaswa kuwa na nafasi ya kununua.
Tofauti ya muhimu baina ya mikataba ijayo na CFD ni muda wa mkataba. Mkataba ujao una tarehe ya mwisho, ambayo baada yake mkataba unapaswa kujadiliwa tena. CFD hazina tarehe ya mwisho na zinaweza kuhitimishwa kwa kipindi cha muda wowote. Haya hivyo, kumbuka kuwa zana zote hizi zinahusika na hatari kubwa ya biashara na zinaweza kulazimisha akaunti yako ya uwekezaji wa rejareja kupoteza fedha isipokuwa kama una mbinu za kutosha za biashara na mpango wa kudhibiti hatari.
CFD zinazohusika kwenye soko la Forex zina misingi ya kodi sawa na jozi za Forex. Kwa maneno mengine, kama wakala ni wa mamlaka za nje, mteja ni wakala wa kodi na yupo huru kulipa kwa matakwa yake binafsi. Mikataba kwa tofauti haina mizigo mingine ya kodi.
Kama mfanyabiashara mwingine, mfanyabiashara wa CFD anafikia mafanikio kwa kujikita kwenye mbinu ya biashara. Kama mfanyabiashara anaweza kufuata sheria zake mwenyewe, mafanikio yatakuja kwa haraka. Njia nyingine zote zitapelekea akaunti za uwekezaji wa rejareja kupoteza fedha kwa haraka kutokana na kiinua mtaji na kukosekana kwa uzoefu na uthibiti mbovu wa hatari.
CFD ni mkataba rasmi uliosanifiwa, kwa hiyo ni mfumo wa kazi halali ya kisheria unaotumika katika miamala ya mabadilishano ya fedha za kigeni au dhamana nyingine za fedha.
Usalama wa biashara ya CFD unahakikishwa kwa mamlaka ya wakala anayetoa kwa wateja wake CFD. Kadiri wakala anavyotegemewa, ndivyo usalama wa mikataba ya tofauti ulivyo. Biashara ya CFD inaweza kuwa salama, lakini kuwa na ujuzi kabla ya kufanya biashara ni muhimu. Upotevu wa fedha kutokana na kiinua mtaji unaweza kuathiri kwa ukubwa msingi wa fedha ya mwekezaji wa rejareja kama hajajiandaa. Biashara ya CFD inahitaji uelewa wa masoko tata, misingi ya uzuiaji wa hatari na uelewa wa kina wa hatari zinazoohusiana nazo, la sivyo, unaweza kujikuta katika hali ya kupoteza fedha kwa haraka kwenye akaunti yako ya uwekezaji ya rejareja.
Ndio. Hizi ni CFD kwa ajili ya masoko ya fedha, kwa mfano, hisa za makampuni ya kigeni ambazo hazipatikani kwa biashara mpaka uwe raia wa nchi inayotoa hisa.
Ukopaji wa mtaji unafanya CFD kufikika na masoko ya fedha ya dunia. Kwa mfano, kufanya biashara katika CFD kwenye hisa kupitia wakala LiteFinance ni asilimia 2% ya mtaji wate wa mali husika. Unahitaji $2.25 kununua hisa ya Apple yenye thamani ya $112. Hata hivyo, unaweza kupoteza fedha wakati wa biashara ya CFD kwa mtaji kama hauna ujuzi na uzoefu wa kutosha.
Tofauti ya bei ya bets na CFDS ni zana tata za fedha ambazo zinaweza kutumika kuinua nafasi katika masoko ya dunia. Ufundi wa ufanyaji kazi wa CFD unatofautiana na jinsi tofauti ya bei ya bets unavyofanya kazi. Tofauti ya bei ya bets ni aina ya pekee ya biashara ya biashara ya dhamana ya fedha inayokuruhusu kubashiri thamani ijayo ya dhamana au mali. Haihusishi umiliki wa mali husika, badala yake inalenga kubashiri mwenendo wa bei. CFDs, kwa upande mwingine, inatoa unyumbulisho na uhodari kwa wafanyabiashara, ikiwaruhusu kwenda ‘juu’ au ‘chini’ katika soko husika kulingana na muonekano wake. Tofauti ya muhimu nyingine baina ya tofauti ya bei ya bets na CFD ni kwamba faida kutoka kwenye tofauti ya bei ya bets haina makato, wakati faida kutoka kwenye biashara ya CFD in ina wajibika katika ongezeko la kodi kwa baadhi ya mamlaka.
P.S. Ulipenda makala yangu? Shiriki kwenye mitandao ya kijamii: itakuwa bora zaidi "asante" :)
Viungo muhimu:
- Ninapendekeza ujaribu kufanya biashara na wakala anayetegemewa hapa. Mfumo huu hukuruhusu kufanya biashara peke yako au kunakili wafanyabiashara waliofaulu kutoka kote ulimwenguni.
- Tumia msimbo wangu wa ofa BLOG kupata bonasi ya amana 50% kwenye jukwaa la LiteFinance. Ingiza tu msimbo huu katika sehemu inayofaa huku ukiweka akaunti yako ya biashara.
- Gumzo la telegramu kwa wafanyabiashara: https://t.me/litefinance. Tunashiriki mawimbi na uzoefu wa biashara
- Kituo cha Telegramu chenye uchanganuzi wa hali ya juu, hakiki za Forex, makala ya mafunzo na mambo mengine muhimu kwa wafanyabiashara https://t.me/litefinance

Maudhui ya chapisho hili yanaelezea maoni ya mwandishi na hayaelezei nafasi ya umuhimu kwa wakala LiteFinance. Nyenzo zilizochapishwa katika kurasa hii zimetolewa kwa nia ya kuto taarifa pekee na hazipaswi kuhusika kama ushauri wa uwekezaji kwa maleno ya Muongozo wa 2014/65/EU.
Kutokana na sheria ya hati miliki, chapisho hili linahusika kama elimu mali, inayohusisha katazo la kunakili na kusambaza bila ya idhini.















































